GOD LOVES YOU/MUNGU ANAKUPENDA

Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

John 3:16 "For God so loved the world that he gave his one and only Son, that whoever believes in him shall not perish but have eternal life.

Sunday, October 28, 2012

UJUMBE: MKARIBISHE YESU KWENYE CHOMBO CHAKO (MESSAGE: INVITE JESUS INTO YOUR VESSEL)

Sunday Sermon with English Translation


Na Mch.: Mwangasa (Resident Pastor)
Maelfu wakisifu na kuabudu katika ibada ya leo (28 0ct.)

Multitudes during today’s services’ praise and worship(28th Oct.)
Mathayo 14:22-33, Yesu alikuwa akiendelea kutenda kazi alizokuja kuzifanya duniani na ukisoma kuanzia Mathayo 14:1-… Utaona aliwalisha watu elfu tano (waume). Na wakati watu wakitaamaki akawalazimisha wanafunzi wake kupanda chomboni ili wavuke bahari. Wanafunzi wake walipokuwa katikati ya bahari ndipo ilipotokea upepo mkali na kuanza kusukasuka chombo. Tuna mmbo mengi ya kujifunza kupitia maandiko haya:-


In the passage of Matthew 14:22-33, we see that Jesus was one who busied Himself with the mission that was bestowed upon Him to accomplish here on earth. In reading from Matthew 14:1, you will see that He fed five thousand people (this figure accounting only for the men that were present). Thereafter, Jesus constrained His disciples to enter into a ship that they should cross over the sea. While His disciples were along this journey though, their ship was tossed about with the waves as a strong wind was upon the sea. There are many things that we can learn from this passage:

HALI YA WANAFUNZI KATIKA CHOMBO: 
(THE DISCIPLES STATE OF AFFAIRS IN THE SHIP):
Ukitafakari kwa makini utaweza kuona hali ya wanafunzi chomboni; inawezekana walishaanza kumlaumu Yesu, au kumlaumu kwa kuwalazimisha kupanda chomboni na yeye asiwemo.

If you were to contemplate, you would begin to come to terms with the disciple’s state of affairs in the ship; it is quite possible in fact that they had began to grumble against Jesus, or grumble against His order for them to enter into the ship without Him accompanying them.
Pia, wanafunzi wa Yesu walikuwa wamekata tama, kwasababu tukio hili lilipotokea mwanzo walikuwa na Yesu chomboni akaukemea upepo lakini mara hii Yesu hakuwepo chomboni. kwa maana hiyo wanafunzi walikuwa katika hofu kuu.


Furthermore, the disciples of Jesus had given up as in a previous sea storm, Jesus was onboard the ship with them. This time round, they were not with Him and as such they were even more petrified and in great distress.

Biblia inasema hata wanafunzi walipomuona Yesu akitembea juu ya maji, wakahisi ni kivuli chake. hapa tunajifunza kuwa kuna wakati kwenye maisha unaweza kuwa unapita kwenye hatua ngumu kimaisha, na kwasababu ya hofu ukajikuta unaiogopa njia ambayo ndio ufumbuzi wa tatizo lako.


The Bible says that when the disciples saw Jesus walking on the water they perceived that it was a spirit. Hear we learn that there are times in life that one may find him or herself enduring a tough season and on account of fear, one will be afraid of a particular appearance or occurrence that will in fact be for their breakthrough.

KWANINI YESU ALITEMBEA JUU YA MAJI:

(WHY DID JESUS WALK ON THE WATER?):

Yawezekana umejiuliza kwanini Yesu alikuja huku akiwa juu ya maji; Kimsingi bahari ndio ambayo ilikuwa tatizo kwa wanafunzi wake, kwahivyo Yesu alikanyaga bahari kuonyesha kuwa  lile tatizo lilikuwa chini ya miguu ya Yesu. Kumbe Yesu yupo juu ya tatizo linalokuzunguka maana lipo chini ya miguu yake.


It could be that you have asked yourself, why did Jesus walk on the water? Principally, the tumultuous sea was the disciple’s key problem, as such Jesus walked on the water to demonstrate that that problem was under His feet. Of a truth, Jesus is above the problem that surrounds you, in other words, your problems are under His feet.

Na ndio maana Petro naye alijaribu kupita juu ya tatizo yaani bahari lakini alipoiangalia bahari alipata hofu. HAPA tunajifunza jambo kwamba hatakiwi kuliangalia tatizo bali mwangalie Yesu ambaye yupo juu ya tatizo.


That is why; Peter attempted to walk on his problem (i.e. the sea) but unfortunately became fearful when he displaced his focus to looking upon the boisterous elements. Here we learn that our focus should not be on our problems but rather on Christ alone who is on top of the problem.

Ukimwamini Yesu unavuka kutoka mautini unaingia uzimani, na Yesu ana mamlaka na funguo za mauti na kuzimu. Hivyo ukiwa kwenye tatizo, usiangalie tatizo bali mwangalie Yesu. unapoelekea kwa Yesu usipepese macho, mtazame Yesu aliyekufa msalabani kwaajili yako.   


If you believe in Jesus you will cross over from death to life; moreover, Jesus has the authority and keys of hell and of death. Therefore when you are in a predicament, do not look upon it but rather fix your focus upon the LORD. In moving toward Him do not shift your gaze, only behold Jesus Christ who died on the cross for you.

 
JAMBO LA KUFANYA UKIWA NDANI YA TATIZO:

(WHAT TO DO WHEN YOU ARE IN A PREDICAMENT):

Katikati ya bahari wanafunzi wakamuona Yesu kama tumaini lao, na ndipo Petro alipoamua kumfuata. kimsingi uamuzi wa Petro kumfuata Yesu kwa kutembea juu ya maji ni sahihi kabisa, ila tatizo ni kwamba petro alitumia uzoefu wake wa bahari ambao ukamfanya asiwaze sauti ya Yesu aliyemuita. watu wengi wameshindwa kutoka ndani ya tatizo kwasababu ya taarifa walizozisikia kutoka kwa watu.


In the midst of the raging seas the disciples saw Jesus as their defense and put their trust in Him, as such Peter was determined to go after Him. Peter’s decision to get to Jesus by walking on the water was a sound one indeed; but the problem was that he relied upon his familiarity of the seas which caused him to disregard the voice of the LORD who had called him. Many people have been unable to break out from their predicament because of what they have been told by others.

Mfano; Mtu ana tatizo la ndoa na ndio limeanza, lakini baada ya kuongea na mtu mwengine mwenye tatizo kama hilo, anamwambia kuwa amedumu kwenye tatizo hilo kwa miaka mingi. Taarifa hiyo moja tu inamfanya huyu ambaye tatizo la ndoa ndio limeanza, akate tamaa na kuingiwa na hofu  kabisa kwa kuhisi naye atadumu kwa miaka hiyo yote.


For example:  a certain newlywed has a marital problem, but after sharing this issue with another person who has a similar problem, the newlywed is told that he or she is rooted therein for the next good couple of years. This single opinion alone is highly likely to cause the newlywed to lose heart and be filled with fear, believing that he or she is stuck for good.

Ni muhimu kujua hakuna haja ya kuangalia tatizo wala watu wengine waliopo kwenye tatizo. tunatakiwa tumuangalie Yesu Kristo ambaye aweza kukutoa kwenye tatizo ulilonalo. unapomwita Yesu kwenye mwili wako uliojaa magonjwa atakapofika yeye yote yatakoma, ukimwita Yesu kwenye ndoa yako yenye matatizo atakapofika tatizo litakama.


It is important to know that there is no need to behold the predicament at hand, neither to look upon others who are also in the same boat. What is needful is for us to look upon Jesus Christ who is able to save from the predicament that one may be facing. When you call the LORD to your sickly body that is filled with disease, when He arrives all issues will cease. When you call the LORD to attend your marital problems, when He arrives the issue will cease.

Isaya 41:9-10 “wewe niikushika toka miisho ya dunia, na kukuita toka pembe zake, nikikuambia, Wewe u mtumishi wangu; nimekuchagua wala sikukutupa; usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwamaana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.”  Kama ukijua jambo ambalo Mungu anataka utend kwenye tatizo utalibadili tatizo hilo na kuwa daraja la kukuvusha na kukupeleka kwenye hatma njema ya maisha yako.


Isaiah 41:9-10:
“Thou whom I have taken from the ends of the earth, and called thee from the chief men thereof, and said unto thee, Thou art my servant; I have chosen thee, and not cast thee away. Fear thou not; for I am with thee: be not dismayed; for I am thy God: I will strengthen thee; yea, I will help thee; yea, I will uphold thee with the right hand of my righteousness.”
If you knew what it was that God has intended to perform toward you in the midst of your predicament, you would give it a substitute title of bridge instead of problem; and it will be the kind of bridge that would take you up and over and toward your life’s pleasant destiny.

Maombi :

Prayer:

Baba Mungu katika Jina la Yesu Kristo leo nimetambua kuwa ninatakiwa nitakiwa nikutazame wewe ninapokuwa kwenye tatizo. ninaomba msamaha kwasababu ya kutazama mambo mengine badala kukutazama wewe Mungu, Mungu naomba unisamehe katika Jina la Yesu.


Father God in the Name of Jesus Christ, today I have discovered that I am to behold you whenever I find myself in any kind of situation. I ask you to forgive me because I have fixed my focus on many other things instead of you oh God, I ask you to forgive me in the Name of Jesus.


 
Katika Jina la Yesu nimeamua kukuita wewe leo, imeandikwa katika Yeremia 3:33 “niite, nami nitakuitikia, name nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.” Leo ninakuita katika Jina la Yesu. Mungu kutoka katika kiti chako cha enzi ninakuita katika Jina la Yesu. Ninakutumaini wewe Mungu katika Jina la Yesu. Natakanivuke na wewe Mungu hadi ng’ambo ya maisha yangu katika Jina la Yesu.


In the Name of Jesus, I have decided to call upon you today, it is written in Jeremiah 33:3, “call unto me, and I will answer thee, and shew thee great and mighty things, which thou knowest not.” Today I call upon you in the Name of Jesus. Oh God, before your throne I call upon the Name of Jesus. I trust in you oh God in the Name of Jesus. I want to cross over with you unto the other side of my life in the name of Jesus.


*picha zote zimechukuliwa katika ibada ya leo*

*All the pictures were taken during today’s service*



MWITE YESU KWENYE TATIZO ULILONALO!!!

INVITE JESUS INTO YOUR SITUATION!!

UFUFUO NA UZIMA {THE GLORY OF CHRIST (T) CHURCH}
TANGANYIKA PACKERS,
Dar es Salaam, TANZANIA

Sunday, October 21, 2012

UJUMBE: MAJESHI YA BWANA {MESSAGE: SOLDIERS OF THE LORD }

Sunday's Sermon with English Translations:
Na Mch. Mwangasa (RP)

With Ps. Mwangasa (RP)

Mchungaji Mwangasa akihubiri neno la Uzima Jumapili hii.

Pastor Mwangasa preaching the word of life this past Sunday

Mwanzo 14:1-16; Kedorlaoma na wafalme wenzake walifanya vita na kufanikiwa kumteka Lutu ambaye alikuwa nduguye Ibrahimu; Mungu akamwambia Ibrahimu kuwa nduguye (Lutu) alikuwa amekamatwa na kutekwa, Ndipo Ibrahimu akaamua kwenda vitani dhidi ya wafalme wale ili kumwokoa nduguye. Baada ya vita akafanikiwa kumkomboa Lutu na kurudisha mali zote zilizokuwa zimeibiwa. Kumbe pamoja na Ibrahimu kuahidiwa Baraka lakini ilimlazimu kupigana vita.



Wachungaji (RP's) wakisikiliza Ibada.

Pastors (RP’s) listening to the sermon

Genesis 14:1-16; During their warfare, King Chedorlaomer and his allied kings took Lot, relative of Abraham captive. God ensured to inform Abraham that his relative (Lot) was captured and carried away, and thus Abraham duly set out to save his relative by launching an offensive against the kings. After his successful warfare, not only was Lot delivered, but all that was plundered was also restored.  We see here that even though Abraham had a promise of blessing, it was still necessary for him to make war.




Vivyo hivyo katika kitabu cha Waefeso 6:10-12; tunagundua kuwa sisi tuliokoka tunatakiwa kupigana vita, ingawa vita vyetu si vya mwilini bali vya rohoni. Kuna wakati unaweza kuona mambo yanaendelea katika ulimwengu wa mwili, na ukafikiri kuwa yanatokea tu lakini kimsingi katika ulimwengu wa roho kuna vita inayoendelea. Shetani alinyang’anywa mamlaka na funguo ya mauti na Yesu alilikabidhi kanisa zile funguo za mauti.

That is why, in the book of Ephesians chapter six, verses ten to twelve (Ephesians 6:10-12) we discover that for those of us who are saved, there is a necessity for us to engage in combat, and yet this warfare of ours is not carnal, but spiritual. There are times when you may deem of things pertaining to the natural life as just mere events but fundamentally in the spiritual realm there is a battle raging. Jesus stripped Satan of authority and snatched from him the keys of death and He bestowed unto the church those keys of death.
Sehemu ya Maelfu ya watu wakiabudu na kusifu katika ibada ya leo Ufufuo na Uzima

Multitudes banding together in praise and worship during today’s service at Resurrection and the Life

Kwa kujua kuwa hana uwezo na amenyang’anywa mamlaka, shetani anatumia wanadamu ili kutimiza lengo lake la kuwadhuru wanadamu. Kimsingi mtu alipuliziwa pumzi na Mungu kwasababu hiyo roho yake ina nguvu (superior) katika ulimwengu wa roho. Hivyo shetani anawatumia hao kutimiza lengo lake la kuwadhuru wanadamu wengine. Kwa hiyo mtu kuwa mchawi maana yake ni kutumiwa na shetani katika kudhuru wanadamu.


Knowing that he has no power and that he has been stripped of authority, Satan uses people in order to fulfill his mission of destroying people. God breathed into man the breath of life and thus his spirit is the superior in the spiritual realm. That is why Satan uses people to destroy people, executing his mission. In effect, a person who practices witchcraft is one who is being used by Satan in order to destroy others.



Hatutakiwi kuwaogopa wachawi kwasababu kama wao wanavyotumiwa na shetani ndivyo sisi tunavyotumiwa na Mungu; na habari nzuri ni kwamba Mungu wetu ni mkuu kuliko shetani. Kumbe kama vile Ibrahimu alipowafuatia Mfalme Kedorlaoma na wenzake na kurudisha vyote, na ndio maana kwa msaada wa Mungu Joshua alisimamisha Jua wakati wakipigana vita.
Platform Choir wakiongoza sifa na Kuabudu Ufufuo na Uzima.

The platform choir leading praise and worship at
The House of Resurrection and the Life


We are not supposed to fear witches because just as they are used by Satan, so we are used by God; and the good news is that our God is sovereign, even over Satan.
In the same way in which Abraham pursued King Cherdolaomer and his allied kings and restored all, Joshua also by the help of God subdued and stopped the sun whilst his battle was raging.



Huwezi kumiliki na kurudisha afya, biashara, kazi au mafanikio uliyonyang’anywa na shetani bila kupigana vita. Kimsingi huwezi kumiliki bila kupigana, shetani ni kama mfalme Kedorlaoma anaweza kuteka na kujimilikisha vile ambavyo Mungu ametuahidia kwa hivyo ili kumiliki ni lazima kufanya vita naye. Kama Mungu alivyomwagiza Ibrahimu kwenda vitani kupambana na waliomteka nduguye ndivyo Yesu ametupa mamlaka ya kupambana na shetani na kumshinda hatimaye kurudisha mali zote.


You cannot take dominion and restore your health, business, career or prosperity which has been plundered from you by Satan without making war. This is a principle, you cannot dominate without battling it out, Satan is like King Chedorlaomer and he can capture and dominate that which God has promised us. Therefore in order to dominate we must make war against him. Just as God commanded Abraham to go to war and contend against those who had taken his relative captive, Jesus has given us authority to contend against Satan and to eventually defeat him, restoring all that had been plundered.

Watu waliokubali kumpa Yesu maisha yao (kuokoka) katika ibada ya Leo
Ufufuo na Uzima

People who made a decision to give their lives to Jesus (get saved) during today’s service at Resurrection and the Life.

Maombi ya Vita:
Baba Katika Jina la Yesu Kristo, umesema lolote tutakalo muomba Mungu kwa Jina la Yesu tutapokea, leo ninasimama kupigana vita katika ulimwengu wa roho. Imeandikwa na alaaniwe azuiaye upanga wake usimwage damu leo ninatumia upanga ambao ni neon la Mungu kuwasambaratisha mapepo wachafu wote, jeshi la giza la wachawi na waganga wanaharibu maisha yangu nina wasambaratisha katika Jina la Yesu.


Father in the Name of Jesus Christ, you said that whatsoever we ask of you oh God in the Name of Jesus, we will receive, today I stand to make war in the spiritual realm. It is written, cursed be he that refrain’s his sword from shedding blood, today I exert the sword, which is the word of God to scatter every unclean spirit, dark forces of sorcerers and witches that are ruining my life, I scatter them in the Name of Jesus.

 

Imaandikwa kwasababu hii mwana wa Adamu alidhihirishwa ili azivunje kazi za ibilisi, leo ninavunja kazi za ibilisi kwenye maisha yangu katika Jina la Yesu. Leo ninawafuata na ninarudisha vyote walivyochukua kwangu Kwa damu ya Yesu Kristo. Afya yangu, mali zangu, nyota yangu na kila jambo walilolichukua kwangu ninarudisha katika Jina la Yesu Kristo.


It is written, for this reason did the son of man appear so that he should destroy the works of the devil, today I destroy the works of the devil over my life in the Name of Jesus. Today I pursue and recover all that was plundered from me by the blood of Jesus Christ. My health, my prosperity, my star and all else that was plunder from me I restore them all in the Name of Jesus.




Ninatangaza ushindi kwenye maisha yangu katika Jina la Yesu, ninatangaza kuwa mali zangu na Baraka zangu zimerudi na ninazifunika katika Jina la Yesu, leo nimeokoka kutoka kwenye mtego wa mwindaji katika Jina la Yesu.


I declare victory over my life in the Name of Jesus, I declare that my prosperity and blessings have been restored and I seal them in the Name of Jesus, today I am delivered from the hunter’s trap in the Name of Jesus.

IBADA KATIKA PICHA (Sunday's Surmon in Pictures):














(we are sorry for the wrong date on pictures;  They were all taken on 21st Oct. 2012)
UFUFUO NA UZIMA (THE GLORY OF CHRIST (T) CHURCH)
TANGANYIKA PACKERS,
KAWE, DAR ES SALAAM.

Monday, October 8, 2012

UJUMBE: NGUVU YA MSAMAHA


Na Mchungaji Yekonia Bihagaze (RP) Jumatatu 8.10.2012
UTANGULIZI:

Mwisho wa somo ili utagundua nguvu iliyopo nyuma ya kusamehe. Kuna watu wanapitia kwenye matatizo na magonjwa kwasababu ya kutokusamehe.

Mathayo 6:9-12 “basi ninyi salini hivi…12 msipowasamehe wengine makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu” Zaburi 103:3 Hapa tunaona kuwa kanuni ya Mungu ni kusamehe kwanza kabla ya kuponya. Na ndio maana waweza kumwona mtu anasema ameokoka lakini bado yupo kwenye ugonjwa kwasababu ya kutokusamehe.

KWANINI UMSAMEHE ALIYEKUKOSEA:

Kumsamehe mtu aliyekuumiza sio jambo la mzaha, na ndio maana kuna watu wanasema kuwa wamesamehe lakini ndani ya mioyo yao bado hajasamehe. Tunatakiwa kusamehe kwasababu kuna nguvu iliyopo nyuma ya mtu aliyekukwaza au kukuumiza.

Watu wengi wanashindwa kusamehe kwasababu hawajui nguvu iliyopo nyuma ya yule mtu aliyewakwaza. Emu tuangalie mfano wa gari; Gari linapomgonga mtu serikali haishtaki gari bali anayeshtakiwa ni dereva. Vivyohivyo ukiumizwa unatakiwa uangalie ile nguvu iliyopo nyuma ya aliyekuumiza. Kimsingi kuna nguvu inayotenda kazi nyuma ya aliyekuumiza na usipoijua hiyo nguvu utajikuta unashindwa kusamehe.

VITU VITATU AMBAVYO NI VIPIMO KAMA UMESAMEHE AU BADO HUJASAMEHE:

1. Ukimsamehe mtu utamwongelea vizuri:

Kama kweli umemsamehe mtu utamwongelea vizuri mbele za watu, kama unasema umemsamehe mtu alafu bado unamwongelea vibaya ujue bado hujasamehe kutoka moyoni mwako. Ukimkuta mtu anaongea mabaya kuhusu mtu aliyemkwaza basi ujue ndani ya moyo wake kuna madabahu ya makwazo na machungu. Na kwasababu hiyo kuna watu wamefukuzwa kazi, wamepigwa kwasababu ya kushindwa kuwanenea watu mazuri.

2. Ukimsamehe mtu utamwombea:

Ishara nyingine kuwa ya kuonyesha kuwa umesamehe ni kumwombea mwingine mazuri; na ndio maana Eliya alipotaka kujenga madhabahu ya Mungu alibomoa kwanza madhabahu ya baali, hata leo huwezi kujenga madhabahu ya Mungu ya amani kama bado moyoni unamadhabahu ya kutokusamehe. Watu wengi wamejikuta wakiomba mabaya kwa watu waliowakosea na kwa namna hiyo wanashindwa kupokea majibu ya matatizo yao.

3. Ukimsamehe mtu utawasiliana kwa uzuri:

Ukimsamehe mtu utawasiliana naye kwa uzuri, nah ii ni kwenye madhabahu ya moyo wako. Hata kama amekujibu vibaya wewe mjibu kwa uzuri. Ni kweli kuwa ukisamehe Yule mtu atakudharau lakini ni muhimu kujua kuwa tunasamehe si kwa ajili ya waliotukosea bali kwa ajili yetu.

Watu wengi wanashindwa kusamehe kwasababu ya kukosa nguvu ya uwezesho ya kuweza kusamehe. Kila mtu aliyeokoka anayo nguvu ya uwezesho ya kusamehe, nayo ni Roho Mtakatifu. Kila mtu aliyeokoka ana Roho Mtakatifu naye hutuwezesha kusamehe, kuokoka kunakupa nguvu ya uwezesho kusamehe. Bila kusamehe huwezi kupokea kutoka kwa BWANA.


MAOMBI YA KUSAMEHE:

Baba katika Jina la Yesu Kristo ninaomba nguvu ya msamaha wako; leo nimetambua kuna nguvu inayotenda kazi nyuma ya mtu aliyenikwanza, leo ninawasamehe wote walionikwaza katika Jina la Yesu. Ninatangaza msamaha, ninavunja madhabahu ya makwazo na kutokusamahe ndani yangu katika jina la Yesu Kristo.

Baba ninaomba uniponye na matatizo yaliyoingia ndani yangu kwasababu ya kutokusamehe katika Jina la Yesu. Leo ninabadilika katika Jina la Yesu. Mimi ni mzima na nimeponywa katika Jina la Yesu.

UFUFUO NA UZIMA (THE GLORY OF CHRIST (T) CHURCH)
TANGANYIKA PACKERS,
KAWE, DAR ES SALAAM.