GOD LOVES YOU/MUNGU ANAKUPENDA

Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

John 3:16 "For God so loved the world that he gave his one and only Son, that whoever believes in him shall not perish but have eternal life.

Sunday, November 11, 2012

UJUMBE: WAKATI WA BWANA


Na Mch. Mwangasa (Resident Pastor) 11/11/2012

Mch. Mwangasa (Resident Pastor)
Akifundisha Neno la Mungu
WAKATI KWA KILA JAMBO:


Mhubiri 3:1-8 “kila jambo kuna majira yake…” Mhubiri 9:11 “Nikarudi na kuona, chini ya jua, si wenye mbio washindao katika michezo… … lakini wakati na bahati huwapata wote”. Biblia inataja kwa kila jambo linalotokea lina majira yake; hakuna jambo linalotokea kama sio wakati wake kutokea. Kwa bahati mbaya sana, wanadamu tunaishi kwa kufuata majira na si majira kuwafuata watu, yaani hatuwezi hatuna jinsi ya kubadili majira, lakini kuna jinsi ya kuishi katika majira tofauti. Watu wengi wamekata tama kwasababu ya kutokujua majira na wakati katika maisha yao.


Platform Team wakimwabudu Mungu
leo wakati wa kusifu na kuabudu


Mhubiri 7:14 “siku ya kufanikiwa hufurahi, na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambasamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asiweze kufahamu jambo lolote litakalofuata baada yake.” Maana ya maneno haya ni kwamba duniani Mungu ameweka mambo mazuri na mabaya pamoja; yaani kuna wakati wa mambo mabaya na saa ya mambo mema. Kwasababu hiyo, watu wameshindwa kujua litakalo fuata mbeleni. Na Mungu amefanya hivi makusudi ili watu wamtafute na kumwomba yeye peke yake.



Tokea siku uliyookoka Mungu  ndiye anayeshughulikia maisha yeko. Na ndio maana unahitaji kujua baada ya kuokoka thamani yako ni kubwa sana; unatakiwa ujue kuwa Mungu anayekushughulikia ndiye muumbaji wa mbingu na nchi; naye ameweka majira na wakati kwa kila jambo.


Wakati wa Kusifu na Kuabudu: UFUFUO NA UZIMA
MAMBO YA KUFANYA KIPINDI UNASUBIRI WAKATI BWANA:


Ukisoma kwa habari ya Hana:

(Angalia.. 1Samweli 1:1-…)  Hana alikaa muda mrefu bila kupata mtoto lakini jambo la muhimu ambalo alifanya ni kwamba, akawa anaenda kuomba huko shilo kila mara. Kumbe pamoja kuwa tunapitia katika wakati mgumu ni muhimu kuomba, watu wengi wameshindwa kupokea na hata kutokujua wakati wao kwasababu wamekuwa hawaombi, wakati wapo katika magumu. Haijalishi, tatizo limechukua muda gani, kwasababu hata tatizo la Hana lilichukua muda mrefu lakini aliendelea kuomba. Ndipo biblia inasema katika mstari wa  20” “ikawa wakati ulipowadia,Hana akachukua mimba akamzaa mtoto mwanaume” kumbe mtoto wa Hana *Samweli, alikuwa anasubiri wakati wake ufike. Tatizo halikuwa kwa Hana, bali wakati ulikuwa bado haujafika. Jambo la kujifunza hapa ni kuwa, wakati Hana anasumbuka kwa kukosa mtoto, alitumia muda ule kuomba. Hili ni jambo la muhimu sana kipindi unasubiri ahadi yako.


Mungu alikuwa ameruhusu Hana apite katika shida ile ili aandike Historia. Wakati mwingine Mungu anaweza kuruhusu upitie wakati mgumu ili utengeneze historia nyingine kwenye maisha yako. Hivyo ni muhimu kujua muda ule unaosubiri muujiza wako unatakiwa ufanye nini. Kama Hana angekatatamaa, Samweli asingekuja leo na hata kama angekuja ingekuwa si kwa kusudi la mwanzo. Subiri wakati wa BWANA, hakuna haja ya kukata tamaa wala kuvunjika moyo.




Kwenye Biblia tunaweza kuona maisha ya Yusufu:

Tunajifunza maisha ya Yusufu ambaye aliota ndoto (angalia Mwanzo 37:5), kuwa mkuu kuliko ndugu zake; ingawa alipitia kipindi kigumu sana, ambacho kama asingesimama na BWANA angekuwa ameshakata tamaa. Yusufu alijua kuwa Mungu ni Mungu wa wakati na majira katika kila jambo. Jambo la kujifunza kwa Yusufu ni kuwa hakutenda dhambi, hata ilipobidi kwenda gerezani kwaajili ya kukwepa dhambi. Kumbe ni muhimu kujilinda na dhambi wakati unamngojea BWANA. (angalia Mwanzo 37-48). Siku zote mawazo ya Mungu sio ya wanadamu, na ndio maana Yusufu aliwaambia ndugu zake kuwa ninyi mliniwazia mabaya lakini Mungu aliniwazia mema.kumbe jambo linguine la kufanya wakati unasubiri ahadi yako kwa Mungu ni kutokutenda dhambi.



Pia tunaweza kujifunza kuhusu jambo hili kupitia Nabii Danieli:

Danieli 9:1-3; Danieli baada ya kusoma kitabu cha tarehe, akafahamu kuwa ulikuwa wakati wa wana wa Israeli kutoka utumwani. Kumbe kuna umuhimu wa kusoma wakati na majira, hata mkulima mzuri ni yule anayejua kusoma majira na wakati. Ndipo Danieli akachukua hatua ya kufunga na kuomba ili kumwomba Mungu watoke utumwani. Jambo la ajabu analokutana nalo ambalo ni kikwazo kingine ni Mkuu wa anga la Uajemi, (angalia Danieli 10:1- … ). Kumbe inawezekana wakati wako ukafika lakini kuna mkuu wa anga (shetani) ambaye amekaa kuzuia. Kuna watu wanapitia wakati mgumu na wa kukatisha tamaa na kumbe kuna mkuu wa anga anayezuiua. Jambo la kufanya ni kupambana na mkuu wa anga hapo lazima wakati wako udhihirike.



Inawezekana umedumu kwenye tatizo kwa muda mrefu sana, umefika hata hali ya kukata tamaa lakini ni muhimu kujua kuwa kila jambo lina wakati wake. BWANA akiamua kutenda kwako, hakuna wa kuzuia kusudi la BWANA.  Unapookoka unatangaza wakati wa BWANA kwenye maisha yako, huu ndio wakati wa BWANA. Hata Yusufu alipita kwenye nyakati tofauti na ngumu lakini wakati wa BWANA ulipotimu aliyaona aliyoahidiwa. Huu ndio wakati wa BWANA kwako na unatakiwa uutangaze katika ulimwengu wa roho. Huwezi kumiliki bila kupigana na mkuu wa anga azuiaye, na kutangaza wakati wa BWANA. Hata Yesu wakati ulipofika alitangaza wakati wa BWANA duniani, tangaza wakati wako katika Jina la YESU. Huu ni wakati wako katika Jina la Yesu.



Translation:


MESSAGE: THE TIMING OF THE LORD

With Ps. Mwangasa (Resident Pastor) 11/11/2012

THERE IS A TIME FOR EVERYTHING:

Ecclesiastes 3:1 To everything there is a season…” [Read Ecclesiastes 3:1-8].
Ecclesiastes 9:11I returned, and saw under the sun, that the race is not to the swift…but time and chance happeneth to them all.”
The Bible tells us that to everything there is a season and that nothing comes to pass outside of its appointed time. Unfortunately though for mankind, we live in step with the seasons, and not the seasons occurring in step with us. There is no means available to mankind to alter the seasons but what there is, is a way in which man can live to cope through the different seasons. Many people have given up because they are unaware of the times and seasons of their lives.

Ecclesiastes 7:14In the day of prosperity be joyful, but in the day of adversity consider: God also hath set the one over against the other, to the end that man should find nothing after him.”
These words demonstrate that in the world God has put both prosperity and adversity, indicating that there is a time for adversity and a time for prosperity. God has allowed this on purpose so that man, in not knowing which lies ahead will entreat Him only.


From the day of your salvation God began to concern Himself with your life. Therefore it is imperative for you to know that from salvation you are of great value and that the God who concerns Himself over you is the creator of the heavens and the earth and He has appointed times and seasons for everything.

WHAT TO DO WHILE WAITING FOR THE TIME OF THE LORD:

In reading up on Hannah:

 (Refer to 1 Samuel 1, from verse one onwards)
Hannah was barren and without child for many years but the notable thing she did was that she ensured to go for prayer at Shiloh at its every appointed time. Despite the hardship that we go through we see here the importance of consistent prayer, many people have not been able to receive and be made aware of what kind of season they are in because they do not pray, her time came about in the midst of her hardship. The duration of the problem does not matter because even Hannah was barren for a long time but she continued in prayer. That is why the Bible says in verse twenty “Wherefore it came to pass, when the time was come about after Hannah had conceived, that she bare a son…” Hannah’s son, Samuel was awaiting his right time to come.
As such the problem was not with Hannah, but rather that her time had not yet come. What we can learn from Hannah is that despite her grief over her barrenness she utilised her time well in prayer. This is a very important thing to do while awaiting your promise.

God allowed Hanna to pass through that problem so that she would make history. Sometimes God can allow for you to endure hardship so that you can attribute a different history to your life. Therefore it is important to know what to do while you are waiting for your miracle from the LORD. If Hannah had given up, Samuel would not have been born and even if he was later born it would have been out of line with God’s original purpose. Wait for the time appointed by the LORD, there is no need to give up or have a broken heart.

From the Bible we can also get an analysis of Joseph’s life:

We can learn from the life of Joseph who dreamt that he was head over his brothers (refer to Genesis 37:5) that despite the hard times that he endured; if he had not held fast unto the LORD he would have given up. Joseph knew that God is a God of times and seasons and that there is a time for everything. What we can learn from Joseph is that he did not sin, and for his refusal to sin he even ended up being imprisoned.  Hear we learn the importance of keeping yourself from sin while awaiting the LORD (refer to Genesis 37 – 48). The thoughts of God are never as those of man, and that is why Joseph told his brothers that even though they had purposed evil toward him God purposed good. So in effect you must ensure not to commit sin while awaiting your promise from the LORD.


Furthermore, we can instruct ourselves about this matter via the Prophet Daniel:

Daniel 9: 1-3
After reading from prophetic records Daniel became aware that it was time for the restoration of Jerusalem. So here we see the great importance in investigating on times and seasons, a good farmer is he who knows how to understand the seasons. It was then that Daniel went forward with fasting and prayer that God should restore Jerusalem. An amazing thing to note of here is the contending of the Prince of Persia (read Daniel chapter ten from verse one). We see that it could be that your time has come but the Prince of the Air (Satan) has positioned himself in opposition. There are people who go through hard and discouraging times but behind it all is the Prince of the Air who is opposing. What needs to be done is warfare against the Prince of the Air and surely then, your time will manifest.


It could be that you have enduring the same problem for a very long time, and you are even at the point of giving up but assuredly that there is a time for everything. When the LORD has purposed to perform something toward you, no amount of opposition can prevent the fulfilment of the purpose of the LORD. When you got saved it was your declaration that it from then it is the LORD’s time in your life, this is the LORD’s time. Even Joseph went through different seasons and hard times but when the time of the LORD came about he saw all that he had been promised. This is the time that the LORD has purposed for you therefore ensure to declare so in the spiritual realm. You cannot dominate without battling against the Prince of the Air who opposes, and to declaring that it is the time of the LORD. Even Jesus when He arrived He declared that it was the time of the LORD on the earth, declare your time in the Name of Jesus. This is your time in the Name of Jesus!



GLORY OF CHRIST (T) CHURCH

UFUFUO NA UZIMA

DAR ES SALAAM

TANZANIA.

Monday, November 5, 2012

UJUMBE: NEEMA YA MUNGU {MESSAGE: THE GRACE OF GOD}

Sunday Sermon's notes with English Translation!!!

   
Na. Mch. Mwangasa {Resident Pastor}      4.11.2012 


TAFSIRI YA NEEMA YA MUNGU KIBIBLIA:

THE BIBLICAL INTERPRETATION OF THE GRACE OF GOD:



Tito 2:11 “maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa…” Waefeso 2:1-10. Kuna tafsiri nyingi sana ya neema ya Mungu; lakini tafsiri ya karibu zaidi inasema neema ni upendeleo wa Mungu kwa mwanadamu ambao hatukuungaramia, tafsri nyingine inasema neema ni daraja kati ya Mungu na wanadamu. Tafsiri nyingine ya neema ya Mungu kwetu ni njia ya Mungu kumfikia mwanadamu kwa njia ya Kristo Yesu.



Titus 2:11 “For the grace of God that bringeth salvation hath appeared to all men…”

Ephesians 2: 1-10

There are many interpretations of the grace of God; but the most accurate states that grace is God’s unmerited favor toward man. Grace has also been interpreted as the bridge between God and man. Another interpretation of God’s grace for us is that it is the path that God takes to get to man, through Christ.



Hata kwenye agano la Kale kulikuwa na tafsiri ya neema mfano utakaposoma katika kitabu cha Mwanzo 6:8  “lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA”. Kimsingi, ulimwengu wa kipindi kile uliokolewa kwasababu ya neema ambayo Nuhu aliipata kwa BWANA. Pia ukisoma katika kitabu cha Yona 4:2; Kwa Tafsiri ya Yona neema ilikuwa ni tabia ya Mungu KWAMBA Mungu ni mwenye rehema na huruma yaani ni kawaida ya Mungu.



Even in the Old Testament we can find a mention of grace, for example when you read Genesis chapter six verse eight (Genesis 6:8)But Noah found grace in the eyes of the LORD.” Principally, those who were saved at that time were saved on account of the grace that Noah had received from the LORD. Furthermore, if you read in the book of John chapter four verse two (John 4:2), John’s definition of grace is that it is the character of God; His compassion and mercy are part and parcel of His nature.



Ukiangalia katika agano jipya tunapata tafsiri nyingine ya neema; Yohana 1:7; kabla ya Kristo upendeleo wa mtu kwa Mungu ulikuwa unapatikana baada ya mtu kutenda matendo mema; lakini Yohana anataja neema kama upendeleo unaokuja bila kugharimia. Kimsingi; ingawa wanadamu walikuwa wametenda dhambi lakini pamoja na dhambi za wanadamu Mungu akaja kumwokoa Mungu, ndio maana katika  Warumi 3:24, Paulo anaeleza kuwa tumepokea ukombozi wa Mungu  bila kugharimia.



Further sifting through the New Testament uncovers another definition of grace, John 1:7. Prior to Christ appearing, an individual’s benevolence and outward righteousness was the only way in which one could obtain the favor of God. But John mentions grace as being unmerited favor. So in effect even though man has sinned, despite this sinful state God came to save man and that is why in Romans 3:24 Paul says that we have received salvation freely.



TUMEOKOLEWA NA NEEMA YA MUNGU:

WE ARE SAVED BY THE GRACE OF GOD:



Kama utapata nafasi ya Kufuatilia Maisha yako utagundua kuna wakati ulipita mahali kwasababu ya neema ya Mungu. Tumepata neema bure.  Unapokuwa umeokoka unakuwa umepokea neema ya Kristo iliyo ya bure; ndio maana hata kama unapitia katika hali ngumu lakini ni muhimu kujua kuna neema ya Mungu iliyo kuu ambayo ni zaidi ya matatizo au magonjwa unayopitia. Hii ndio maana ya lile andiko katika Tito 2:11 “maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa…” Neema ya Mungu yatutosha.



In taking time to reminisce upon your life, you will discover that there were times that it was only by the grace of God that you managed to make it through. Grace has freely been bestowed upon us. In that you are saved, it is that you have received this free grace of Christ; that is why even if you are enduring great hardship it is important to know that there exists the grand grace of God which is greater the problems or sickness that you are enduring. This is what is meant in Titus 2:11For the grace of God that bringeth salvation hath appeared to all men…” God’s grace is all sufficient.



Hakuna haja ya kuangalia watu wanakuita nani kwasababu hata kipindi cha Yusufu watu walimwona mfungwa mbakaji lakini Neema ya Mungu ilimwita kuwa ni waziri mkuu wa Misri. Ingawa alipitia kwenye wakati mgumu lakini bado neema ya Mungu ilimwita waziri Mkuu. Unapoona hayo ni muhimu kutenga muda wa kumshukuru Mungu kila siku, unapoliona jua linawaka yupo anayesababisha liwake mshukuru Mungu kwa neema yake.



There is no need for you to be concerned with the name-calling being people hurled at you because even in Joseph’s days, people labeled him prisoner and rapist but it was the grace of God that instead called him Prime Minister of Egypt. Despite the hardships he endured, the grace of God still called him Prime Minister. In beholding this it thus becomes important to put aside time to for thanksgiving every day; for us just to see the sun rise is enough reason to give thanks to God for His grace.



NEEMA YA WOKOVU:

GRACE OF SALVATION:



Hii ni neema iliyondani ya watu waliompokea Yesu Kristo. Wakati wengine wakipitia matatizo wanaenda kwa waganga wa dunia hii sisi tuliompokea Yesu Kristo tuna neno la ushindi (kwa kupigwa kwake sisi tumepona Isaya 53:5). Unapokuwa umeokoka yaani umempokea Yesu Mungu anakufanya uwe mtoto wake hivyo anakuwa anataka kila unachokitenda kiwe nembo ya utukufu wake.



This is the grace which is within those who have received Christ Jesus. While the people of this world consult with sorcerer’s and witches for their hardships, we who have received Jesus Christ have the words of victory: by His stripes, we are healed (Isaiah 53:5). When you are saved (when you have received Jesus) God makes you His child and as such he desires for His glory to be displayed in all that you do.



Kumbe ukiokoka unakuwa umepokea neema ya Mungu lakini hatuwezi kutenda dhambi kwasababu kuna neema. Neema inatuagiza kuishi maisha matakatifu. Mungu hachanganywi na dhambi. Inawezekana unapitia katika hali ngumu kimaisha lakini jambo la kujua ni kuwa neema ya Mungu yakutosha. Tuna neema ya Mungu sisi tuliompokea Yesu Kristo kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yetu.



In effect when you are saved you have received the grace of God, but because there is grace we must not use it as an excuse for committing sin. Grace commands us to live a holy life. God does not mix with sin. It could be that you are going through a hard time in life but it is imperative to know that God’s grace is sufficient. For those of us who have received Jesus as LORD and Savior of our lives, we have the grace of God.
THE GLORY OF CHRIST (T) CHURCH

KAWE, DAR ES SALAAM,
TANZANIA.

Friday, November 2, 2012

Somo: Roho ya ufahamu na hekima.

Na Mchungaji: Adriano Makazi (RP)

Isaya 11:1~2
1 Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.
2 Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana;

Mambo mchache ya kufahamu.
-shetani huzifumba fahamu za watu waoumbwa kwa sura na mfano wa Mungu ili wasizijue haki zao.
-kwenye bustani ya edeni nyoka alimdanganya Hawa akamwambia ukila matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya utakuwa Kama Mungu
-lakini tayari waliumbwa kwa mfano na sura ya Mungu
Imeandikwa mtaifahamu kweli nayo kweli itawaweka huru (Yohana 8:32)
1 Yohana
2. Cor 4:3-4....mungu wa dunia amepofusha fikila zao wasio amini ili isiwazukie nuru ya injili iliyo sura yake Mungu

Yohana 1:1~5
1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.
Neno ni Mungu
Neno ni Yesu
Neno ni mkate
Neno ni njia
Neno linaweza kuvaa mwili

YOHANA 1:14
14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

(..."kila aliye mkiri Yesu ni mwana wa Mungu ,,,,,Mungu yuko ndani yako....")
Ukizishika amiri zake watatu watakuja kukaa kwako.
i). Mungu baba.
ii). Mungu mwana.
iii). Mungu Roho Mtakatifu

YOHANA 14:21~23
21 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.
22 Yuda (siye Iskariote), akamwambia, Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu?
23 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
(.....Tamani Mungu afanye MAKAO kwako.....")

 Mdhihilishe Yesu kwa watu waliokuzunguka usimfungie Yesu ndani ya box.

GODSON ISSA NEW SNP MOROGORO



 Mchungaji kiongozi Wa Kanisa la GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH maarufu kwa Jina la  UFUFUO NA UZIMA amempaka mafuta Dr Godson Issa Zacharia kuwa Mchungaji kiongozi Wa Kanisa Hilo huko Morogoro.. Mchungaji Godson amechukua nafasi ya Mchungaji FRANK ANDREW ambaye amerejea makao makuu Jijini Dar Es Salaam.

Mch. Kiongozi Josephat Gwajima akimweka wakfu Mchungaji Dr Godson Issa
kuwa Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Morogoro.
*Picha na Rp Bihagaze (Ufufuo Crew Group on Facebook)*

Sunday, October 28, 2012

UJUMBE: MKARIBISHE YESU KWENYE CHOMBO CHAKO (MESSAGE: INVITE JESUS INTO YOUR VESSEL)

Sunday Sermon with English Translation


Na Mch.: Mwangasa (Resident Pastor)
Maelfu wakisifu na kuabudu katika ibada ya leo (28 0ct.)

Multitudes during today’s services’ praise and worship(28th Oct.)
Mathayo 14:22-33, Yesu alikuwa akiendelea kutenda kazi alizokuja kuzifanya duniani na ukisoma kuanzia Mathayo 14:1-… Utaona aliwalisha watu elfu tano (waume). Na wakati watu wakitaamaki akawalazimisha wanafunzi wake kupanda chomboni ili wavuke bahari. Wanafunzi wake walipokuwa katikati ya bahari ndipo ilipotokea upepo mkali na kuanza kusukasuka chombo. Tuna mmbo mengi ya kujifunza kupitia maandiko haya:-


In the passage of Matthew 14:22-33, we see that Jesus was one who busied Himself with the mission that was bestowed upon Him to accomplish here on earth. In reading from Matthew 14:1, you will see that He fed five thousand people (this figure accounting only for the men that were present). Thereafter, Jesus constrained His disciples to enter into a ship that they should cross over the sea. While His disciples were along this journey though, their ship was tossed about with the waves as a strong wind was upon the sea. There are many things that we can learn from this passage:

HALI YA WANAFUNZI KATIKA CHOMBO: 
(THE DISCIPLES STATE OF AFFAIRS IN THE SHIP):
Ukitafakari kwa makini utaweza kuona hali ya wanafunzi chomboni; inawezekana walishaanza kumlaumu Yesu, au kumlaumu kwa kuwalazimisha kupanda chomboni na yeye asiwemo.

If you were to contemplate, you would begin to come to terms with the disciple’s state of affairs in the ship; it is quite possible in fact that they had began to grumble against Jesus, or grumble against His order for them to enter into the ship without Him accompanying them.
Pia, wanafunzi wa Yesu walikuwa wamekata tama, kwasababu tukio hili lilipotokea mwanzo walikuwa na Yesu chomboni akaukemea upepo lakini mara hii Yesu hakuwepo chomboni. kwa maana hiyo wanafunzi walikuwa katika hofu kuu.


Furthermore, the disciples of Jesus had given up as in a previous sea storm, Jesus was onboard the ship with them. This time round, they were not with Him and as such they were even more petrified and in great distress.

Biblia inasema hata wanafunzi walipomuona Yesu akitembea juu ya maji, wakahisi ni kivuli chake. hapa tunajifunza kuwa kuna wakati kwenye maisha unaweza kuwa unapita kwenye hatua ngumu kimaisha, na kwasababu ya hofu ukajikuta unaiogopa njia ambayo ndio ufumbuzi wa tatizo lako.


The Bible says that when the disciples saw Jesus walking on the water they perceived that it was a spirit. Hear we learn that there are times in life that one may find him or herself enduring a tough season and on account of fear, one will be afraid of a particular appearance or occurrence that will in fact be for their breakthrough.

KWANINI YESU ALITEMBEA JUU YA MAJI:

(WHY DID JESUS WALK ON THE WATER?):

Yawezekana umejiuliza kwanini Yesu alikuja huku akiwa juu ya maji; Kimsingi bahari ndio ambayo ilikuwa tatizo kwa wanafunzi wake, kwahivyo Yesu alikanyaga bahari kuonyesha kuwa  lile tatizo lilikuwa chini ya miguu ya Yesu. Kumbe Yesu yupo juu ya tatizo linalokuzunguka maana lipo chini ya miguu yake.


It could be that you have asked yourself, why did Jesus walk on the water? Principally, the tumultuous sea was the disciple’s key problem, as such Jesus walked on the water to demonstrate that that problem was under His feet. Of a truth, Jesus is above the problem that surrounds you, in other words, your problems are under His feet.

Na ndio maana Petro naye alijaribu kupita juu ya tatizo yaani bahari lakini alipoiangalia bahari alipata hofu. HAPA tunajifunza jambo kwamba hatakiwi kuliangalia tatizo bali mwangalie Yesu ambaye yupo juu ya tatizo.


That is why; Peter attempted to walk on his problem (i.e. the sea) but unfortunately became fearful when he displaced his focus to looking upon the boisterous elements. Here we learn that our focus should not be on our problems but rather on Christ alone who is on top of the problem.

Ukimwamini Yesu unavuka kutoka mautini unaingia uzimani, na Yesu ana mamlaka na funguo za mauti na kuzimu. Hivyo ukiwa kwenye tatizo, usiangalie tatizo bali mwangalie Yesu. unapoelekea kwa Yesu usipepese macho, mtazame Yesu aliyekufa msalabani kwaajili yako.   


If you believe in Jesus you will cross over from death to life; moreover, Jesus has the authority and keys of hell and of death. Therefore when you are in a predicament, do not look upon it but rather fix your focus upon the LORD. In moving toward Him do not shift your gaze, only behold Jesus Christ who died on the cross for you.

 
JAMBO LA KUFANYA UKIWA NDANI YA TATIZO:

(WHAT TO DO WHEN YOU ARE IN A PREDICAMENT):

Katikati ya bahari wanafunzi wakamuona Yesu kama tumaini lao, na ndipo Petro alipoamua kumfuata. kimsingi uamuzi wa Petro kumfuata Yesu kwa kutembea juu ya maji ni sahihi kabisa, ila tatizo ni kwamba petro alitumia uzoefu wake wa bahari ambao ukamfanya asiwaze sauti ya Yesu aliyemuita. watu wengi wameshindwa kutoka ndani ya tatizo kwasababu ya taarifa walizozisikia kutoka kwa watu.


In the midst of the raging seas the disciples saw Jesus as their defense and put their trust in Him, as such Peter was determined to go after Him. Peter’s decision to get to Jesus by walking on the water was a sound one indeed; but the problem was that he relied upon his familiarity of the seas which caused him to disregard the voice of the LORD who had called him. Many people have been unable to break out from their predicament because of what they have been told by others.

Mfano; Mtu ana tatizo la ndoa na ndio limeanza, lakini baada ya kuongea na mtu mwengine mwenye tatizo kama hilo, anamwambia kuwa amedumu kwenye tatizo hilo kwa miaka mingi. Taarifa hiyo moja tu inamfanya huyu ambaye tatizo la ndoa ndio limeanza, akate tamaa na kuingiwa na hofu  kabisa kwa kuhisi naye atadumu kwa miaka hiyo yote.


For example:  a certain newlywed has a marital problem, but after sharing this issue with another person who has a similar problem, the newlywed is told that he or she is rooted therein for the next good couple of years. This single opinion alone is highly likely to cause the newlywed to lose heart and be filled with fear, believing that he or she is stuck for good.

Ni muhimu kujua hakuna haja ya kuangalia tatizo wala watu wengine waliopo kwenye tatizo. tunatakiwa tumuangalie Yesu Kristo ambaye aweza kukutoa kwenye tatizo ulilonalo. unapomwita Yesu kwenye mwili wako uliojaa magonjwa atakapofika yeye yote yatakoma, ukimwita Yesu kwenye ndoa yako yenye matatizo atakapofika tatizo litakama.


It is important to know that there is no need to behold the predicament at hand, neither to look upon others who are also in the same boat. What is needful is for us to look upon Jesus Christ who is able to save from the predicament that one may be facing. When you call the LORD to your sickly body that is filled with disease, when He arrives all issues will cease. When you call the LORD to attend your marital problems, when He arrives the issue will cease.

Isaya 41:9-10 “wewe niikushika toka miisho ya dunia, na kukuita toka pembe zake, nikikuambia, Wewe u mtumishi wangu; nimekuchagua wala sikukutupa; usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwamaana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.”  Kama ukijua jambo ambalo Mungu anataka utend kwenye tatizo utalibadili tatizo hilo na kuwa daraja la kukuvusha na kukupeleka kwenye hatma njema ya maisha yako.


Isaiah 41:9-10:
“Thou whom I have taken from the ends of the earth, and called thee from the chief men thereof, and said unto thee, Thou art my servant; I have chosen thee, and not cast thee away. Fear thou not; for I am with thee: be not dismayed; for I am thy God: I will strengthen thee; yea, I will help thee; yea, I will uphold thee with the right hand of my righteousness.”
If you knew what it was that God has intended to perform toward you in the midst of your predicament, you would give it a substitute title of bridge instead of problem; and it will be the kind of bridge that would take you up and over and toward your life’s pleasant destiny.

Maombi :

Prayer:

Baba Mungu katika Jina la Yesu Kristo leo nimetambua kuwa ninatakiwa nitakiwa nikutazame wewe ninapokuwa kwenye tatizo. ninaomba msamaha kwasababu ya kutazama mambo mengine badala kukutazama wewe Mungu, Mungu naomba unisamehe katika Jina la Yesu.


Father God in the Name of Jesus Christ, today I have discovered that I am to behold you whenever I find myself in any kind of situation. I ask you to forgive me because I have fixed my focus on many other things instead of you oh God, I ask you to forgive me in the Name of Jesus.


 
Katika Jina la Yesu nimeamua kukuita wewe leo, imeandikwa katika Yeremia 3:33 “niite, nami nitakuitikia, name nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.” Leo ninakuita katika Jina la Yesu. Mungu kutoka katika kiti chako cha enzi ninakuita katika Jina la Yesu. Ninakutumaini wewe Mungu katika Jina la Yesu. Natakanivuke na wewe Mungu hadi ng’ambo ya maisha yangu katika Jina la Yesu.


In the Name of Jesus, I have decided to call upon you today, it is written in Jeremiah 33:3, “call unto me, and I will answer thee, and shew thee great and mighty things, which thou knowest not.” Today I call upon you in the Name of Jesus. Oh God, before your throne I call upon the Name of Jesus. I trust in you oh God in the Name of Jesus. I want to cross over with you unto the other side of my life in the name of Jesus.


*picha zote zimechukuliwa katika ibada ya leo*

*All the pictures were taken during today’s service*



MWITE YESU KWENYE TATIZO ULILONALO!!!

INVITE JESUS INTO YOUR SITUATION!!

UFUFUO NA UZIMA {THE GLORY OF CHRIST (T) CHURCH}
TANGANYIKA PACKERS,
Dar es Salaam, TANZANIA

Sunday, October 21, 2012

UJUMBE: MAJESHI YA BWANA {MESSAGE: SOLDIERS OF THE LORD }

Sunday's Sermon with English Translations:
Na Mch. Mwangasa (RP)

With Ps. Mwangasa (RP)

Mchungaji Mwangasa akihubiri neno la Uzima Jumapili hii.

Pastor Mwangasa preaching the word of life this past Sunday

Mwanzo 14:1-16; Kedorlaoma na wafalme wenzake walifanya vita na kufanikiwa kumteka Lutu ambaye alikuwa nduguye Ibrahimu; Mungu akamwambia Ibrahimu kuwa nduguye (Lutu) alikuwa amekamatwa na kutekwa, Ndipo Ibrahimu akaamua kwenda vitani dhidi ya wafalme wale ili kumwokoa nduguye. Baada ya vita akafanikiwa kumkomboa Lutu na kurudisha mali zote zilizokuwa zimeibiwa. Kumbe pamoja na Ibrahimu kuahidiwa Baraka lakini ilimlazimu kupigana vita.



Wachungaji (RP's) wakisikiliza Ibada.

Pastors (RP’s) listening to the sermon

Genesis 14:1-16; During their warfare, King Chedorlaomer and his allied kings took Lot, relative of Abraham captive. God ensured to inform Abraham that his relative (Lot) was captured and carried away, and thus Abraham duly set out to save his relative by launching an offensive against the kings. After his successful warfare, not only was Lot delivered, but all that was plundered was also restored.  We see here that even though Abraham had a promise of blessing, it was still necessary for him to make war.




Vivyo hivyo katika kitabu cha Waefeso 6:10-12; tunagundua kuwa sisi tuliokoka tunatakiwa kupigana vita, ingawa vita vyetu si vya mwilini bali vya rohoni. Kuna wakati unaweza kuona mambo yanaendelea katika ulimwengu wa mwili, na ukafikiri kuwa yanatokea tu lakini kimsingi katika ulimwengu wa roho kuna vita inayoendelea. Shetani alinyang’anywa mamlaka na funguo ya mauti na Yesu alilikabidhi kanisa zile funguo za mauti.

That is why, in the book of Ephesians chapter six, verses ten to twelve (Ephesians 6:10-12) we discover that for those of us who are saved, there is a necessity for us to engage in combat, and yet this warfare of ours is not carnal, but spiritual. There are times when you may deem of things pertaining to the natural life as just mere events but fundamentally in the spiritual realm there is a battle raging. Jesus stripped Satan of authority and snatched from him the keys of death and He bestowed unto the church those keys of death.
Sehemu ya Maelfu ya watu wakiabudu na kusifu katika ibada ya leo Ufufuo na Uzima

Multitudes banding together in praise and worship during today’s service at Resurrection and the Life

Kwa kujua kuwa hana uwezo na amenyang’anywa mamlaka, shetani anatumia wanadamu ili kutimiza lengo lake la kuwadhuru wanadamu. Kimsingi mtu alipuliziwa pumzi na Mungu kwasababu hiyo roho yake ina nguvu (superior) katika ulimwengu wa roho. Hivyo shetani anawatumia hao kutimiza lengo lake la kuwadhuru wanadamu wengine. Kwa hiyo mtu kuwa mchawi maana yake ni kutumiwa na shetani katika kudhuru wanadamu.


Knowing that he has no power and that he has been stripped of authority, Satan uses people in order to fulfill his mission of destroying people. God breathed into man the breath of life and thus his spirit is the superior in the spiritual realm. That is why Satan uses people to destroy people, executing his mission. In effect, a person who practices witchcraft is one who is being used by Satan in order to destroy others.



Hatutakiwi kuwaogopa wachawi kwasababu kama wao wanavyotumiwa na shetani ndivyo sisi tunavyotumiwa na Mungu; na habari nzuri ni kwamba Mungu wetu ni mkuu kuliko shetani. Kumbe kama vile Ibrahimu alipowafuatia Mfalme Kedorlaoma na wenzake na kurudisha vyote, na ndio maana kwa msaada wa Mungu Joshua alisimamisha Jua wakati wakipigana vita.
Platform Choir wakiongoza sifa na Kuabudu Ufufuo na Uzima.

The platform choir leading praise and worship at
The House of Resurrection and the Life


We are not supposed to fear witches because just as they are used by Satan, so we are used by God; and the good news is that our God is sovereign, even over Satan.
In the same way in which Abraham pursued King Cherdolaomer and his allied kings and restored all, Joshua also by the help of God subdued and stopped the sun whilst his battle was raging.



Huwezi kumiliki na kurudisha afya, biashara, kazi au mafanikio uliyonyang’anywa na shetani bila kupigana vita. Kimsingi huwezi kumiliki bila kupigana, shetani ni kama mfalme Kedorlaoma anaweza kuteka na kujimilikisha vile ambavyo Mungu ametuahidia kwa hivyo ili kumiliki ni lazima kufanya vita naye. Kama Mungu alivyomwagiza Ibrahimu kwenda vitani kupambana na waliomteka nduguye ndivyo Yesu ametupa mamlaka ya kupambana na shetani na kumshinda hatimaye kurudisha mali zote.


You cannot take dominion and restore your health, business, career or prosperity which has been plundered from you by Satan without making war. This is a principle, you cannot dominate without battling it out, Satan is like King Chedorlaomer and he can capture and dominate that which God has promised us. Therefore in order to dominate we must make war against him. Just as God commanded Abraham to go to war and contend against those who had taken his relative captive, Jesus has given us authority to contend against Satan and to eventually defeat him, restoring all that had been plundered.

Watu waliokubali kumpa Yesu maisha yao (kuokoka) katika ibada ya Leo
Ufufuo na Uzima

People who made a decision to give their lives to Jesus (get saved) during today’s service at Resurrection and the Life.

Maombi ya Vita:
Baba Katika Jina la Yesu Kristo, umesema lolote tutakalo muomba Mungu kwa Jina la Yesu tutapokea, leo ninasimama kupigana vita katika ulimwengu wa roho. Imeandikwa na alaaniwe azuiaye upanga wake usimwage damu leo ninatumia upanga ambao ni neon la Mungu kuwasambaratisha mapepo wachafu wote, jeshi la giza la wachawi na waganga wanaharibu maisha yangu nina wasambaratisha katika Jina la Yesu.


Father in the Name of Jesus Christ, you said that whatsoever we ask of you oh God in the Name of Jesus, we will receive, today I stand to make war in the spiritual realm. It is written, cursed be he that refrain’s his sword from shedding blood, today I exert the sword, which is the word of God to scatter every unclean spirit, dark forces of sorcerers and witches that are ruining my life, I scatter them in the Name of Jesus.

 

Imaandikwa kwasababu hii mwana wa Adamu alidhihirishwa ili azivunje kazi za ibilisi, leo ninavunja kazi za ibilisi kwenye maisha yangu katika Jina la Yesu. Leo ninawafuata na ninarudisha vyote walivyochukua kwangu Kwa damu ya Yesu Kristo. Afya yangu, mali zangu, nyota yangu na kila jambo walilolichukua kwangu ninarudisha katika Jina la Yesu Kristo.


It is written, for this reason did the son of man appear so that he should destroy the works of the devil, today I destroy the works of the devil over my life in the Name of Jesus. Today I pursue and recover all that was plundered from me by the blood of Jesus Christ. My health, my prosperity, my star and all else that was plunder from me I restore them all in the Name of Jesus.




Ninatangaza ushindi kwenye maisha yangu katika Jina la Yesu, ninatangaza kuwa mali zangu na Baraka zangu zimerudi na ninazifunika katika Jina la Yesu, leo nimeokoka kutoka kwenye mtego wa mwindaji katika Jina la Yesu.


I declare victory over my life in the Name of Jesus, I declare that my prosperity and blessings have been restored and I seal them in the Name of Jesus, today I am delivered from the hunter’s trap in the Name of Jesus.

IBADA KATIKA PICHA (Sunday's Surmon in Pictures):














(we are sorry for the wrong date on pictures;  They were all taken on 21st Oct. 2012)
UFUFUO NA UZIMA (THE GLORY OF CHRIST (T) CHURCH)
TANGANYIKA PACKERS,
KAWE, DAR ES SALAAM.

Monday, October 8, 2012

UJUMBE: NGUVU YA MSAMAHA


Na Mchungaji Yekonia Bihagaze (RP) Jumatatu 8.10.2012
UTANGULIZI:

Mwisho wa somo ili utagundua nguvu iliyopo nyuma ya kusamehe. Kuna watu wanapitia kwenye matatizo na magonjwa kwasababu ya kutokusamehe.

Mathayo 6:9-12 “basi ninyi salini hivi…12 msipowasamehe wengine makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu” Zaburi 103:3 Hapa tunaona kuwa kanuni ya Mungu ni kusamehe kwanza kabla ya kuponya. Na ndio maana waweza kumwona mtu anasema ameokoka lakini bado yupo kwenye ugonjwa kwasababu ya kutokusamehe.

KWANINI UMSAMEHE ALIYEKUKOSEA:

Kumsamehe mtu aliyekuumiza sio jambo la mzaha, na ndio maana kuna watu wanasema kuwa wamesamehe lakini ndani ya mioyo yao bado hajasamehe. Tunatakiwa kusamehe kwasababu kuna nguvu iliyopo nyuma ya mtu aliyekukwaza au kukuumiza.

Watu wengi wanashindwa kusamehe kwasababu hawajui nguvu iliyopo nyuma ya yule mtu aliyewakwaza. Emu tuangalie mfano wa gari; Gari linapomgonga mtu serikali haishtaki gari bali anayeshtakiwa ni dereva. Vivyohivyo ukiumizwa unatakiwa uangalie ile nguvu iliyopo nyuma ya aliyekuumiza. Kimsingi kuna nguvu inayotenda kazi nyuma ya aliyekuumiza na usipoijua hiyo nguvu utajikuta unashindwa kusamehe.

VITU VITATU AMBAVYO NI VIPIMO KAMA UMESAMEHE AU BADO HUJASAMEHE:

1. Ukimsamehe mtu utamwongelea vizuri:

Kama kweli umemsamehe mtu utamwongelea vizuri mbele za watu, kama unasema umemsamehe mtu alafu bado unamwongelea vibaya ujue bado hujasamehe kutoka moyoni mwako. Ukimkuta mtu anaongea mabaya kuhusu mtu aliyemkwaza basi ujue ndani ya moyo wake kuna madabahu ya makwazo na machungu. Na kwasababu hiyo kuna watu wamefukuzwa kazi, wamepigwa kwasababu ya kushindwa kuwanenea watu mazuri.

2. Ukimsamehe mtu utamwombea:

Ishara nyingine kuwa ya kuonyesha kuwa umesamehe ni kumwombea mwingine mazuri; na ndio maana Eliya alipotaka kujenga madhabahu ya Mungu alibomoa kwanza madhabahu ya baali, hata leo huwezi kujenga madhabahu ya Mungu ya amani kama bado moyoni unamadhabahu ya kutokusamehe. Watu wengi wamejikuta wakiomba mabaya kwa watu waliowakosea na kwa namna hiyo wanashindwa kupokea majibu ya matatizo yao.

3. Ukimsamehe mtu utawasiliana kwa uzuri:

Ukimsamehe mtu utawasiliana naye kwa uzuri, nah ii ni kwenye madhabahu ya moyo wako. Hata kama amekujibu vibaya wewe mjibu kwa uzuri. Ni kweli kuwa ukisamehe Yule mtu atakudharau lakini ni muhimu kujua kuwa tunasamehe si kwa ajili ya waliotukosea bali kwa ajili yetu.

Watu wengi wanashindwa kusamehe kwasababu ya kukosa nguvu ya uwezesho ya kuweza kusamehe. Kila mtu aliyeokoka anayo nguvu ya uwezesho ya kusamehe, nayo ni Roho Mtakatifu. Kila mtu aliyeokoka ana Roho Mtakatifu naye hutuwezesha kusamehe, kuokoka kunakupa nguvu ya uwezesho kusamehe. Bila kusamehe huwezi kupokea kutoka kwa BWANA.


MAOMBI YA KUSAMEHE:

Baba katika Jina la Yesu Kristo ninaomba nguvu ya msamaha wako; leo nimetambua kuna nguvu inayotenda kazi nyuma ya mtu aliyenikwanza, leo ninawasamehe wote walionikwaza katika Jina la Yesu. Ninatangaza msamaha, ninavunja madhabahu ya makwazo na kutokusamahe ndani yangu katika jina la Yesu Kristo.

Baba ninaomba uniponye na matatizo yaliyoingia ndani yangu kwasababu ya kutokusamehe katika Jina la Yesu. Leo ninabadilika katika Jina la Yesu. Mimi ni mzima na nimeponywa katika Jina la Yesu.

UFUFUO NA UZIMA (THE GLORY OF CHRIST (T) CHURCH)
TANGANYIKA PACKERS,
KAWE, DAR ES SALAAM.