Mchungaji Kiongozi: Josephat Gwajima. 14. 9. 2012
Kuanzia mwanzo wa wiki hii
tumekuwa tukijifunza kuhusu mikataba inayotokana na maneno; na tuliona kuwa
maneno yaweza kuleta mikataba, na hasa tulijifunza zaidi juu ya maneno
anayotamka mtu binafsi; Pia tuliona maandiko kadhaa Mithali 6:2; na pia tukaona
kuwa uweza wa laana au baraka upo katika maneno ambayo mtu anatamka Kumbukumbu
la torati 30:15, 19; hivyo tulijikita zaidi katika mikataba ya maneno mtu
anayojitamkia. Leo tutaona maneno ambayo mtu anatamkiwa na mtu mwingine.
MANENO YA KUTAMKIWA NA LAANA:
Mwanzo 9:18-29; kuna mambo ya
kuangalia; Hamu baba wa Kanaani akauona uchi wa baba yake, akaenda kuwaambia
nduguze ( ukiangalia hapa nani mwenye kosa waweza sema ni aliyelewa na kukaa
uchi) Lakini wanawe wengine wawili walipomuona wakamfunika baba yao. Lakini
katika Mstari wa 25’ Nuhu katoka kwenye ulevi, akamlaani mototo wa aliyemuona
akiwa uchi.
Tunaona hapa, tatizo kubwa
lilikuwa Hamu kuwaelezea wenzake kuwa baba yake yuko uchi. Lakini Nuhu
alimlaani Kanaani ambaye ni mototo wa Hamu; na wana wakanaani ndio wanaotajwa
katika kitabu cha Mwanzo 10:15-20;
Kutoka 3:8; Kutoka 23:23; Joshua 24:11. Hii laana ya Kanaani ndiyo iliyokuja
kuwadhuru watoto wake yaani Wahivi, Wakanaani, Wayebusi na hii ndiyo laana
inayowatafuna. Lakini ukiangalia mwanzo ilianzia kwenye maneno ambayo Nuhu
alitamka kwa wajukuu wake.
LAANA INATENDAJE KAZI:
Waefeso 6:1 “ Enyi watoto watiini
wazazi wenu katika BWANA, maana hii ndiyo haki”; kimsingi watu anawazi wa
rohoni na wa mwilini; wazazi wa rohoni wanaitwa Wazazi katika BWANA. Na katika Waefeso 6:2 “waheshimu baba na mama
yako, uwe na heri…” Neno hili uwe na
heri… linatajwa kwenye biblia ya kingereza
kuwa “It may be well with you” YAANI ili mambo yakuendee vizuri; hivyo
kumbe kuna uwezekano wa mtu kuwa anaenenda vibaya kwasababu ya kutokuwaheshimu
wazazi. Na hapa ndipo Nuhu alitamka maneno ya Laana kwa watoto wake na
yakatimia.
Sasa kitu kinachotokea ni kwamba;
Yesu alisema “maneno niwaambiayo ni roho tena ni uzima” na pia biblia inasema “Kila
andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho” kumbe kuna maneno yenye pumzi
au roho ya shetani. Na ndio maana waweza kumuombea mtu kwa maneno na akafufuka
kwasababu maneno yale ni roho. Hivyo kama ukimkosea mzazi akatamka maneno juu
yako, yale maneno kwakuwa ni mabaya, mashetani yanakuwa nyuma ya yake ili wasimamie
yatimie. Hivyo nyuma ya maneno kuna roho, aidha ya roho takatifu au roho chafu.
“KAMA UNATAKA KUWA MTU WA MUNGU
MZURI; TUMIA MANENO YAKO VIZURI”
ROHO ILIYO NYUMA YA MANENO:
Mpaka hapa tumeona kuna roho
nyuma ya maneno; na ndio maana Hesabu 14:28-29 Mungu anasema nitawatendea yale
ninayo yasikia mnasema, kumbe maneno ambayo mtu anayatamka yana nguvu nyuma
yake ya kuweza kutokea. Sasa maneno mabaya
yanapotamkwa juu ya mtu; mashetani wanachofanya ni kuyachukua maneno hayo na
kuyatimiza kwa mtu aliyetamkiwa. Mfano mzazi
akikutamkia maneno labda hutazaa, utakuwa kichaa, hutafilisika au tutaona
utakapooa. Hayo maneno yanaweza kuwa kifungo kwenye maisha ya mtu.
Na ndio maana katika kitabu cha
Mithali 26:2; Biblia inasema, “…laana isyo na sababu haimpigi mtu…” kwaiyo
kumbe kama laana inasababu itatenda kazi bila shaka. Kwasabu kuna mashetani
wanasimamia laana. Na ukiangalia kwa habari ya Elisha na Naamani, Baada ya
Naamani kutakaswa alitaka kumpa hela Elisha,
Elisha akakataa lakini baada ya muda mtumishi wa Elisha Gehazi akaenda
kwa Naamani na kutaka mali kwako, matokeo yake Elisha alipojua kwa roho wa
Mungu,; akamtamkia kuwa uwe na ukoma. Na kuanzia saa ile Gehazi akawa na Ukoma.
Kumbe mtu awezakuwa kwenye kifungo kwasababu ya maneno aliyowahi kutamkiwa.
Kumbe; kuna watu wapo kwenye
vifungo vya magonjwa, kutokuzaa, kutokuolewa au matatizo mbalimbali kwasababu
ya maneno ya kutamkiwa. Kumbukumbu 28:15-. Hapo zinatajwa laana nyingi hapo,
kumbe laana hata za maneno zaweza kuja kwa namna ya matatizo, kupungukiwa,
kushindwa, kukata tama n.k. Inawezekana wewe hukutamkiwa maneno, lakini baba au
mama yako alitamkiwa ulipokuwa tumboni ni muhimu kuvunja maneno hayo.
MAOMBI BAADA YA SOMO:
Baba Katika Jina la Yesu Kristo;
leo ninasimama kinyume na maneno yote niliyotamkiwa, katika Jina la Yesu. Maneno
ya kushindwa, ya kukata tama au ya kutokufanikiwa, ninafuta maneno yote kwa
Jina la Yesu. Ninafuta maneno niliyotamkiwa nikiwa mdogo ninayafuta kwa Jina la
Yesu. Ninaamuru maneno hayo yote hayatatimia katika Jina la Yesu. Yeyote aliyatamka
awe baba, au mama au mtu yeyote; ninayafuta maneno niliyotamkiwa kwenye ndoa,
kwenye mahusiano ninayafuta Katika Jina la Yesu.
Kazi iliyopotea kwasababu ya
maneno ya kutamkiwa, niaamuru uarudishwe katika Jina la Yesu. Ninakataa kupoteza
katika Jina la Yesum nikipata nimepata katika Jina La Yesu. Ninatangaza ushindi na mafanikio kwenye maisha
yangu katika Jina la Yesu, natangaza Baraka Juu yangu kwa Jina la Yesu.
No comments:
Post a Comment