Danieli 3:1-30; 6:10-; tumesoma habari mbili ambazo zinawahusu kwa ukaribu watu wane yaani, Danieli, Meshaki, Shedraka na Abednego. Kipindi kile Babeli walivamia Yerusalemu na kuwachukua waisraeli utumwani, na kati yao wakachukuliwa watu kadhaa kwenda kufanya kazi za mfalme, baadhi ya waliokuwepo ni hawa wane. Kupitia hao tunapata kujifunza:-
Habari ya Kwanza kuhusu Sanamu iliyowekwa na Mfalme Nebkadneza: (Danieli 3:1-30):
Mtoto akitoa ushuhuda baada ya Maombezi |
Jambo la ajabu likatokea pale
mfalme alipowatupa kwenye moto, maana moto uliwalamba na kuwateketeza wale
walioenda kuwatupa. Lakini wao hawakuungua, moto haukuwaweza kabisa. Lakini jambo la muhimu kujifunza kupitia
habari hii. Pata picha ya hali iliyokuwepo kwa hawa watu watatu, maana lilikuwa
ni jambo gumu kwao. Wangetarajia Mungu awaokoe mapema yaani Mungu asingeruhusu
watupwe kwenye moto.
Kwanza; Mungu alitaka atimize neon
lake alilonena kupitia nabii Isaya KWAMBA “Upitapo
katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha;
uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.” Isaya 43:2,
Mungu wetu ni moto ulao, na kwakulithibitisha hilo akaruhusu hadi wafikie
dakika ya mwisho, ili ajichukulie utukufu wake.
Pili; Mungu huwa anaokoa dakika
ya mwisho, pale unapohisi kuwa huna msaada mwingine ndipo Mungu anajichukulia
utukufu; watu wengi wanakata tama mapema bila kujua kuwa Mungu huokoa katika
saa ambayo hukuitarajia, Wakina Shedraka wangetarajia Mungu awaokoe katika
hatua ya kwanza, lakini Mungu alikuja kwao dakika ya mwisho.
Tatu; tunaona watu walioenda
kuwashtaki kwa Mfalme; hapa tunajifunza kuwa unapoishi kuna watu watasema, kuna
watu watakupinga, kuna watu watakushtaki kwa waganga wa kienyeji wakitaka
kukuangamiza. Lakini ni muhimu kujua kuwa Mungu wetu ni Mungu wa kuokoa.
Unapookoka Mungu anakuwa pamoja na wewe.
Nne; ndani ya moto kulikuwa na
mtu wane; Yesu Kristo yupo pamoja nasi, imeandikwa, “wa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu;” 1 Yohana
5:4, hakuna moto ambao umeanzishwa na wanadamu, utakaoweza kukushinda. Sisi
tumezaliwa na Mungu, na lazima tuushinde ulimwengu. Ni kweli unaweza kuwa
unapitia kunye tatizo ambalo limekuwa moto kwenye maisha yako, lakini jambo la
muhimu kujua kwamba, Hakuna moto uliofanywa na wanadamu utakaoweza kukushinda,
kwasababu maana baada ya kuokoka unakuwa umezaliwa na Mungu.
Habari ya pili kuhusu, Danieli na
Mfalme Dario: (Danieli 6:10-28):
Katika kipindi cha Mfalme Dario,
watu kadhaa wakaamua kwa hila kumuangamiza Danieli, na hawakuona jambo lolote
la kumuangamiza isipokuwa kwa habari ya Mungu wake. Imeandikwa, “Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na
maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme;
na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote,
au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme
atatupwa katika tundu la simba.” Hivyo, Mfalme akaweka muhuri kwenye sharia,
lakini Danieli bila kujua ile sharia yeye akaendelea na Ibada kama kawaida; wakati
huohuo, liliandaliwa ntanuru la samba ambao nao hawakupewa chakula kwa muda wa
siku saba. Lakini cha ajabu kuwa walipomtupa ndani ya shimo wale samba hawakuweza
kumdhuru. Ndipo mfalme akaamuru wale waliopangia hila watupwe wao. Ambapo samba
waliwadaka hewani kabla ya kufika chini. Katika habari hii kuna mambop kadhaa
ya kujifunza:-
Kwanza; Simba wakagoma kumla Danieli; biblia inasema, “Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye malaika wake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa miali ya moto.” Waebrania 1:7. Mungu anasema hutufanya sisi watumishi wake kuwa miale ya moto, n wale samba walimuona danieli kama mwali wa moto hivyo hawakuweza kumrarua. Unapookoka unakuwa mwali wa moto katika ulimwengu wa roho na hakuna silaha inayoweza kukudhuru.
Pili; Danieli alikuwa mtu wa
kabila la Yuda na kwaabari ya Yuda kuna Simba wa kabila la Yuda, samba wasingeweza
kumdhuru, kwa kuwa Danieli alikuwa pamoja na Mungu aliye simba wa kabila la
Yuda. Hakuna haja ya kuogopa yale magumu unayopitia,. Kwa kuwa ndani yako kuna simba
wa kabila la Yuda yaani Yesu Kristo. Pamoja na kukosa chakula kwa muda wa siku
saba, hawakuweza kumla Danieli mtu wa Mungu.
Tatu; baada ya Mfalme kugundua
kuwa samba wameshindwa kumuua Danieli, ndipo akaamuru wale waliotaka kumuua
Danieli kwa hila waingize wao shimoni. Likatimia andiko kuwa, “Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani
yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka
atamwuma.” Mhubiri 10:8, wale waliokuandalia kifo au aibu kwa hila,
itamrudia mwenyewe. Mungu huwaondoa wenye haki kwenye ajali na kuwaweka waovu
badala yake. Wanakupiga vita kwa hila
usiangaike we mwangalie Mungu, yeye atakupigania.
Unapokuwa unaomba, inabidi ujue
kuwa upo na Mungu awezaye kutenda kwa namna ya ajabu sana; Yoshua 10:9 “Bwana naye akawatapanya mbele ya Israeli, naye Israeli
akawaua uuaji ulio mkuu hapo Gibeoni, akawafukuza waikimbilie hiyo njia ya
kukwelea kwenda Bethhoroni, na kuwapiga hata kufikilia Azeka, tena hata
kufikilia Makeda. Kisha ikawa, hapo walipokuwa wakimbia mbele ya Israeli, hapo
walipokuwa katika kutelemkia Bethhoroni, ndipo Bwana alipowatupia mawe makubwa
kutoka mbinguni juu yao hata kufikilia Azeka, nao wakafa; hao waliokufa kwa
kuuawa na hayo mawe ya barafu walikuwa ni wengi kuliko hao waliouawa na wana wa
Israeli kwa upanga.” Mungu aliwahi kuwaangushia mawe, maadui wa Israeli,
Unatakiwa ujue BWANA amewatia adui zako mikononi mwako uwatende unavyotaka. Unatakiwa
ujue hauko peke yako Mungu yupo kwaajili yako, kukuokoa. Mungu kwetu sisi ni
Mungu wa kuokoa na njia za kutoka mautini zina yeye!!!
Glory Of Christ (T) Church
Ufufuo na Uzima
Dar es Salaam, Tanzania.
very blessing mass,nimemiss kweli kanisa la Ufufuo na uzima Mbarikiwe sana
ReplyDelete