GOD LOVES YOU/MUNGU ANAKUPENDA

Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

John 3:16 "For God so loved the world that he gave his one and only Son, that whoever believes in him shall not perish but have eternal life.

Friday, September 14, 2012

MIKATABA YA ITOKANAYO NA MANENO ANAYOKUTAMKIA MTU


Mchungaji Kiongozi: Josephat Gwajima.     14. 9. 2012


Utangulizi:
Kuanzia mwanzo wa wiki hii tumekuwa tukijifunza kuhusu mikataba inayotokana na maneno; na tuliona kuwa maneno yaweza kuleta mikataba, na hasa tulijifunza zaidi juu ya maneno anayotamka mtu binafsi; Pia tuliona maandiko kadhaa Mithali 6:2; na pia tukaona kuwa uweza wa laana au baraka upo katika maneno ambayo mtu anatamka Kumbukumbu la torati 30:15, 19; hivyo tulijikita zaidi katika mikataba ya maneno mtu anayojitamkia. Leo tutaona maneno ambayo mtu anatamkiwa na mtu mwingine.

MANENO YA KUTAMKIWA NA LAANA:
Mwanzo 9:18-29; kuna mambo ya kuangalia; Hamu baba wa Kanaani akauona uchi wa baba yake, akaenda kuwaambia nduguze ( ukiangalia hapa nani mwenye kosa waweza sema ni aliyelewa na kukaa uchi) Lakini wanawe wengine wawili walipomuona wakamfunika baba yao. Lakini katika Mstari wa 25’ Nuhu katoka kwenye ulevi, akamlaani mototo wa aliyemuona akiwa uchi.

Tunaona hapa, tatizo kubwa lilikuwa Hamu kuwaelezea wenzake kuwa baba yake yuko uchi. Lakini Nuhu alimlaani Kanaani ambaye ni mototo wa Hamu; na wana wakanaani ndio wanaotajwa katika kitabu cha  Mwanzo 10:15-20; Kutoka 3:8; Kutoka 23:23; Joshua 24:11. Hii laana ya Kanaani ndiyo iliyokuja kuwadhuru watoto wake yaani Wahivi, Wakanaani, Wayebusi na hii ndiyo laana inayowatafuna. Lakini ukiangalia mwanzo ilianzia kwenye maneno ambayo Nuhu alitamka kwa wajukuu wake.

LAANA INATENDAJE KAZI:
Waefeso 6:1 “ Enyi watoto watiini wazazi wenu katika BWANA, maana hii ndiyo haki”; kimsingi watu anawazi wa rohoni na wa mwilini; wazazi wa rohoni wanaitwa Wazazi katika BWANA.  Na katika Waefeso 6:2 “waheshimu baba na mama yako, uwe na heri…”  Neno hili uwe na heri… linatajwa kwenye biblia ya kingereza  kuwa “It may be well with you” YAANI ili mambo yakuendee vizuri; hivyo kumbe kuna uwezekano wa mtu kuwa anaenenda vibaya kwasababu ya kutokuwaheshimu wazazi. Na hapa ndipo Nuhu alitamka maneno ya Laana kwa watoto wake na yakatimia.

Sasa kitu kinachotokea ni kwamba; Yesu alisema “maneno niwaambiayo ni roho tena ni uzima” na pia biblia inasema “Kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho” kumbe kuna maneno yenye pumzi au roho ya shetani. Na ndio maana waweza kumuombea mtu kwa maneno na akafufuka kwasababu maneno yale ni roho. Hivyo kama ukimkosea mzazi akatamka maneno juu yako, yale maneno kwakuwa ni mabaya, mashetani yanakuwa nyuma ya yake ili wasimamie yatimie. Hivyo nyuma ya maneno kuna roho, aidha ya roho takatifu au roho chafu.
“KAMA UNATAKA KUWA MTU WA MUNGU MZURI; TUMIA MANENO YAKO VIZURI”

ROHO ILIYO NYUMA YA MANENO:
Mpaka hapa tumeona kuna roho nyuma ya maneno; na ndio maana Hesabu 14:28-29 Mungu anasema nitawatendea yale ninayo yasikia mnasema, kumbe maneno ambayo mtu anayatamka yana nguvu nyuma yake ya kuweza kutokea.  Sasa maneno mabaya yanapotamkwa juu ya mtu; mashetani wanachofanya ni kuyachukua maneno hayo na kuyatimiza kwa mtu aliyetamkiwa.  Mfano mzazi akikutamkia maneno labda hutazaa, utakuwa kichaa, hutafilisika au tutaona utakapooa. Hayo maneno yanaweza kuwa kifungo kwenye maisha ya mtu.

Na ndio maana katika kitabu cha Mithali 26:2; Biblia inasema, “…laana isyo na sababu haimpigi mtu…” kwaiyo kumbe kama laana inasababu itatenda kazi bila shaka. Kwasabu kuna mashetani wanasimamia laana. Na ukiangalia kwa habari ya Elisha na Naamani, Baada ya Naamani kutakaswa alitaka kumpa hela Elisha,  Elisha akakataa lakini baada ya muda mtumishi wa Elisha Gehazi akaenda kwa Naamani na kutaka mali kwako, matokeo yake Elisha alipojua kwa roho wa Mungu,; akamtamkia kuwa uwe na ukoma. Na kuanzia saa ile Gehazi akawa na Ukoma. Kumbe mtu awezakuwa kwenye kifungo kwasababu ya maneno aliyowahi kutamkiwa.

Kumbe; kuna watu wapo kwenye vifungo vya magonjwa, kutokuzaa, kutokuolewa au matatizo mbalimbali kwasababu ya maneno ya kutamkiwa. Kumbukumbu 28:15-. Hapo zinatajwa laana nyingi hapo, kumbe laana hata za maneno zaweza kuja kwa namna ya matatizo, kupungukiwa, kushindwa, kukata tama n.k. Inawezekana wewe hukutamkiwa maneno, lakini baba au mama yako alitamkiwa ulipokuwa tumboni ni muhimu kuvunja maneno hayo.

MAOMBI BAADA YA SOMO:
Baba Katika Jina la Yesu Kristo; leo ninasimama kinyume na maneno yote niliyotamkiwa, katika Jina la Yesu. Maneno ya kushindwa, ya kukata tama au ya kutokufanikiwa, ninafuta maneno yote kwa Jina la Yesu. Ninafuta maneno niliyotamkiwa nikiwa mdogo ninayafuta kwa Jina la Yesu. Ninaamuru maneno hayo yote hayatatimia katika Jina la Yesu. Yeyote aliyatamka awe baba, au mama au mtu yeyote; ninayafuta maneno niliyotamkiwa kwenye ndoa, kwenye mahusiano ninayafuta Katika Jina la Yesu.

Kazi iliyopotea kwasababu ya maneno ya kutamkiwa, niaamuru uarudishwe katika Jina la Yesu. Ninakataa kupoteza katika Jina la Yesum nikipata nimepata katika Jina La Yesu.  Ninatangaza ushindi na mafanikio kwenye maisha yangu katika Jina la Yesu, natangaza Baraka Juu yangu kwa Jina la Yesu.

UFUFUO NA UZIMA {THE GLORY OF CHRIST (T) CHURCH}
TANGANYIKA PACKERS,
KAWE, DAR ES SALAAM 


No comments:

Post a Comment