Na Mchungaji Kiongozi
Josephat Gwajima
Utangulizi:
Wakristo wengi huwa hawazungumzii neno kafara kwasababu
wanahisi kuwa ni la waganga wa kienyeji, lakini hili neno limeandikwa kwenye
biblia mara nyingi sana. Hii ni kuonyesha kuwa
wapo watu wanatoa kafara.
KAFARA KWENYE BIBLIA:
Baada ya Yoshua na wana wa Israeli kuangusha ukuta wa Yeriko,
Yoshua aliweka agano kuwa atakayeamua kujenga ukuta ataanza kwa kufiwa na
mwanawe wa kwanza na akasema akimaliza atafiwa na mwanae wa pili. Yoshua 6:20-27. Lakini miaka mingi
baadaye mtu mmoja akatoa kafara ya wanawe ili aweze kujenga ngome ya Yeriko kwa
upya, Kumbe kafara yaweza kutolewa kwa ajili ya kujenga kitu duniani. Imeandikwa
katika 1Wafalme 16:38.
2Wafalme 3:20-27, Hapa tunaona habari ya Huyu Mfalme ambaye
baada ya kuona anashindwa vita dhidi ya wana wa Israeli, akaamua kumtoa kafara
mwanaye na hilo jambo likawa hasira juu ya Israeli na kashinda vita. Kumbe
kafara inaweza ikamwezesha mtu kushinda vita. Ukisoma maandiko haya kwa haraka
hutoweza kuelewa lakini ukikaa ukatafakari utaona kuna jambo la muhimu sana hapo.
Kafara ya mtu kwenye biblia; 2Wafalme17:17,“Wakawapitisha
watoto wao, waume na wake, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza
nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, hata kumkasirisha” kumpitisha mtoto motoni ni kumchoma
moto kama kafara yaani ukisoma biblia ya kingereza inatumia neno “sacrifices “ Ezekieli 16:20-21, kumbe jambo la
kafara lipo kwenye biblia,na hapa Ezekieli anasema wakawatoa kafara wanao kuwa
chakula; na pia neno hili limeoneka na pia katika kitabu cha Ezekieli 20:31-32.
KWELI KUHUSU KAFARA:
Mtoto au mtu akitolewa kafara anakuwa ameuwawa Mwili na
kupewa majini au mashetani, katika biblia shetani anayehusika na mambo ya kafara,
Mambo ya Walawi 18:21; ukisoma biblia
ya Kiswahili unaweza ukahisi moleki ni mtu lakini tuangalie kwenye biblia ya
kingereza “do not give out your children to be sacrifices..” Mambo ya Walawi 20:2 “who sacrifices.. kumbe inawezekana unaumwa na upo kwenye ugonjwa
kumbe ndio unatolewa kafara hivyo..
Kumbe sasa waweza
kumwona mtu amekufa na ugonjwa Fulani kumbe ni kafara, mwingine anatoa
kafara kwa ajili ya utajiri. Mambo ya Walawi
20:3, pia tunaona kuwa kumbe wachawi hawa wanatoa ndugu na si mtu ambaye
hamjui. Yaani kama una ndugu wa karibu au wa mbali ambaye ni mchawi, Yule ndiye
anayeweza kukutoa kafara, na kwenye kitabu cha Mambo ya walawi shetani aliyekuwa anahusika na kafara aliitwa Moleki. Walawi 20:4,5 2Wafalme 20:10
Hayo maandiko ni ya agano la kale lakini pia katika agano
jipya jambo hili limetajwa pia; 2Wakorintho
10:20 “.”
KWANINI WATU WANATOA
KAFARA:
Ukiangalia habari ya Nuhu baada ya kutoka kwenye safina nuhu
alimtolea Mungu sadaka na ile harufu ilipofika kwa Mungu; akasema hatailaani
nchi tena kumbe ile harufu ina maana sana kwenye ulimwengu wa roho; vivyo hivyo
wanapo mtolea shetani kafara wanalenga kumpa ile harufu na ile harufu inamfanya
shetani awa tekelezee wanayohitaji. Mtu anamtoa mwanawe ili kuwapa kafara
mashetani, wamtekelezee anacho hitaji kama utajiri n.k.
Mambo ya Walawi 2:12 “Vitu hivyo mtavisongeza kwa Bwana kuwa ni malimbuko; lakini
visifike juu ya madhabahu kuwa ni harufu ya kupendeza.” Utajiuliza hii
harufu na sadaka; hapa ni kafara inayotolewa kwa mashetani. Mambo ya Walawi 3:15, 16, Hesabu 5:17, Sadaka
ya vinywaji hii ni baadhi ya mila hapa kwetu ni pale mtu anakunywa pombe alafu
anawapulizia watu, hii ndio inaitwa sadaka ya vinywaji inayotolewa. Sasa hii
inapotolewa kwa mashetani kwenye ulimwengu wa roho wanakuja mahali pale. Hesabu 15:10; 17:24; 18:7
KUWA MAKINI NA KAFARA ZILIZOTOLEWA KWA
MASHETANI:
Kumbe
shetani anaweza kutolewa kafaraza aina mbalimbali inaweza kuwa ya vinywaji, uji,
nafaka, harufu, watoto au watu wazima; na ni muhimu kuwa makini sana na
kuhudhuria sherehe ambazo si za ki Mungu kwasababu waweza kujikuta unashiriki
kwenye sadaka hiyo. Kuna watu ambao matatizo yao yamewaanza baada ya kushiriki
chakula cha kafara jambo hili biblia imekataza kwasababu ya madhara yake.
Ufunuo 5:8; 8:3 hapa biblia inataja sadaka ya harufu, na ndio
maana ukienda kwenye maduka mengi utakuta wameweka vitu vinaitwa ubani; Hii ni
sadaka au kafala ya kuteketezwa kwa majini, Isaya 43:23; Yeremia 6:20; 17:26, Ubani na Udi ni sadaka ya
kuteketezwa, kimsingi; ile harufu ndiyo inayoifanya iitwe sadaka ya kuteketezwa,
kwahiyo mtu unayemuona anachoma ubani ni anakuwa anatoa kafara ya ubani. Nehemia 13:9.. sadaka za unga na sadaka
za ubani. Kimsingi watu tuliookolewa hatutoi sadaka za ubani kwasababu biblia
inasema maombi ya watakatifu ndio sadaka ya harufu kwa Mungu. (Yohana 19:39)
Kumbe
unapoona mahali au duka ukakuta wanachoma udi kimsingi ni kwamba wanaita Mashetani
ambayo yanawasaidia kuleta wateja. Na ndio maana maduka mengi yana kuwa na vitu
hivi ambavyo ni kafara au sadaka ya harufu; ili majini yaite wateja. Na ndio
maana watu wengi wenye majini wanapenda ubani kwasababu kile ndio chakula chao.
KAFARA YA NCHI:
Kuna
uwezekano nchi ikawekewa kafara ili wananchi wasiongee, yaani kunakuwa na
matatizo katika nchi lakini kumbe ni kwasababu ya kuwaita mashetani ili kufanya
wananchi wasidai haki yao. Na ndio maana kuna vitu ambavyo vinapitishwa kwenye nchi
ambavyo kwa hakika ni kafara ya harufu kwa shetani. Mambo kama mwenge unaopita
ni sadaka kwa mashetani kwa ajili ya nchi, kama unahitaji kujua ukweli wa jambo
hili muombe Mungu akuonyeshe; katika ulimwengu wa roho, utajua wazi kuwa ni
kafara kabisa kwa ajili ya nchi nzima.
Biblia
iko wazi kuhusu kafara inayotolewa kwa ajili ya nchi; Katika biblia Kumbukumbu La Torati 32:43 “Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake; Kwa maana
atatwaa kisasi kwa damu ya watumwa wake, Atawatoza kisasi adui zake, Tena atafanya kafara kwa nchi yake, na watu
wake.” Kumbe kuna uwezakano wa nchi kutolewa kafara yaani mtu anatoa
sadaka ili kuita mashetani kwenye nchi. Ni muhimu unapokuwa unaomba uwe
unavunja na kusambaratisha kafara zilizo tolewa katika nchi. Nchi ya Tanzania
inatakiwa ikombolewe kutoka kwenye kafala.
NGUVU YA KAFARA:
Unaweza
ukajiuliza kafara inafanyaje kazi; kimsingi; sadaka au kafara ya vinywaji, damu
au vyote tulivyoona ni chakula cha mashetani. Na kimsingi mashetani yapo katika
ngazi mbalimbali kuanzia majoka mpaka kwenye majini majini madogo; kwahiyo
wachawi au washirikina huita mashetani kulingana na ukubwa wa kafara kama
ikitolewa kafara ya kuku anakuja shetani wa ngazi ndogo. Na ikitolewa kafara
kubwa kama ya mtu inaliita shetani la ngazi ya juu sana. Hivyo kama mtu
hajaokoka ni rahisi kutolewa kafara kwasababu anakuwa hana ulinzi wa Mungu.
TANGANYIKA PACKERS,
KAWE, DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment