GOD LOVES YOU/MUNGU ANAKUPENDA

Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

John 3:16 "For God so loved the world that he gave his one and only Son, that whoever believes in him shall not perish but have eternal life.

Monday, September 24, 2012

UJUMBE: VIUMBE NA MAUMBILE HEWA.

Na Mchungaji Kiongozi: Josephat Gwajima. Tarehe 17.6.2012

UTANGULIZI:-

Viumbe ni vilivyo umbwa , vyaweza kuwa wanadamu, vitu maji, anga na vitu vingine vyote, na Mumbile ni mtazamo au jinsi viumbe hivyo vinavyoonekana. Ni Muhimu kujua viumbe vya kiroho vinaweza kuvaa maumbile tofauti. Ndio maana Yesu alipofufuka, Mariam mama yake alimuona na kuhisi ni mtunza bustani utajuuliza kwanini mama yake hakumtambua kirahisi na wakati alikuwa naye muda wa kutosha, hii ni kwasababu Yesu alijibadili na kuwa kama mtunza bustani, na mariam akahisi ni mtunza bustani.

ROHO ZINAWEZA KUVAA MAUMBE : Kibiblia:-

Unaposoma kitabu cha mwanzo ni muhimu kujua kuwa kimeelezea kuhusu asili ya ulimwengu, mwanzo wa vitu vyote. Emu tuangalie kwa undani MWANZO 3:1-24.. HII NI HABARI YA Adamu na Hawa walipokula tunda, katika mstari wa 13 Hawa akasema "nyoka alinidanganya" lakini nyoka huyuhuyu ndio anaitwa shetani. Kumbe tangu kitabu cha mwanzo (asili) kinadhihirisha kuwa kuna uwezekano wa shetani (wa rohoni) kuvaa umbo la nyoka. Kama shetani angemtokea hawa kwa umbo lake la asili, asingefanikiwa kumdanganya hivyo ilimlazimu avae mwili. Sasa kumbe uwezekano wa kuvaa umbo upo.

Maandiko yanayoonyesha uwezekano huo:-
 • ZABURI 91:13 utajiuliza kwanini biblia inasema "utakanyaga nyoka au simba".. ukichambua kwa akili ya rohoni jambo hili; Utagundua kuwa Biblia inaonyesha uwezekano wa viumbe wa rohoni kuvaa miili.
 • LUKA 10:19 Biblia inaonyesha maumbo; kumbe unaweza kuona mtu anasema. "ugonjwa huu ulinianza nilipoumwa na mdudu" na ndio maana Mungu ametupa mamlaka ya kukanyaga nyoka na ng'e kwasababu  shetani aweza kuvaa maumbile ya hivyo vitu.
 • MARKO 16:18; Biblia inasema hata ukinywa kitu cha kufisha; yaani sumu kumbe shetani aweza kujibadili na kuwa sumu.
• ISAYA 27:1 Kumbe Biblia inaonyesha kuwa kunanyoka aliye baharini na ndio maana utaona kuna ajali zinatokea baharini, kumbe kuna shetani limejigeuza na kuwa joka baharini.

mara nyingi shetani hutenda kazi kwa kujibadilisha na kuwa kiumbe chochote ili kukuangusha, au kukufuatilia au kukutoa kwenye kusudi la Mungu. Ni muhimi kama mtu uliyeokoka kuwa makini na kujua kuwa shetani aweza kujibadili na kuwa umbo lolote ili akuteke.

SHETANI AWEZA KUJIBADILI MAUMBILE MBALIMBALI

Shetani anaweza kujibadili maumbile kwa ajili ya kutimiza azma yake aliyoikusudia, shetani akiamua kumteka mtu anaweza kutumia mtu, kitu, mti, gari au kitu chochote kutimiza azma yake. Na ndio maana Joshua alipokutana na mtu asiyemjua akamuuliza “je wewe ni wa upande wetu” Na mtu huyu alikuwa rohoni si mwilini tunaweza kuona katika kitabu cha JOSHUA 5:13-15, Joshua alijua kuwa kuna uwezekano wa shetani kujibdili katika maumbile mbalimbali. Ndio maana kwa watu walioko mikoa ya shinyanga wanajua kunavijiji wanavyoita Gamboshi, ni miji yenye watu lakini ya kichawi, yaani mapepo na mashetani wamejibadili na kuwa mji. Kumbe shetani aweza kujibadili.

KUTOKA 8:6-7 tunaona hapa kuwa Haruni alinyoosha fimbo na kutokea vyura, juu ya nchi ya Misri, na waganga wa misri wakafanya vilevile kuleta vyura juu ya nchi, utajiuliza kwanini hawa waganga waliweza kuleta vyura.. ni kwasababu shetani anaweza kujibadili kwenda kwenye maumbo mbalimbali.

UFUNUO 13:10. Yohana aliona katika ulimwengu wa roho, maumbo ya wanyama mbalimbali yote hii ni kudhihirisha kuwa shetani anaweza kujibadili, UFUNUO 13:6. shetani hapa ameonekana kama mnyama aliyetoka baharini, kimsingi yeye shetani ni roho lakini anaweza kuvaa maumbo mbalimbali ili kutenda kazi katika kutimiza azma yake. Ni muhimu kukataa na kuangamiza maumbo yote ambayo shetani anatumia ili kukushambulia. “deactivate them in The Name Of Jesus”

Na ndio maana ni rahisi mtu kukwambia, ugonjwa ulimwanza baada ya kupaliwa. kumbe shetani amegeuka na kuwa kitu cha kumpalia mtu ili kupitisha ugonjwa huo na kumfanya mtu ahisi kuwa kile kitu ndio kimesababisha. Hata kipindi cha Yesu walipokuwa wanavuka baharini na mashua ukaja upepo mkali na ukataka kuangusha kile chombo, lakini Yesu akaukemea na upepo ukatulia. Kimsingi Yule ni shetani alijibadili na kuwa upepo ili kuwazuia wasihubiri injili.

MIJI YA ROHONI.

UFUNUO 21:2 hapa tunaona kuwa Yohana aliona mji wa rohoni. Ufunuo 21:10 huu mji ambao Yohana aliona na haupo kwenye ulimwengu wa mwili na huwezi kuuona kimwili. Huu mji sio wa mwilini kwasababu Yohana akasema “ akanichukua katika roho” maana yake hakuwa katika ulimwengu wa mwili bali wa Rohoni. Na ndio maana hata shetani huiga “imitator” na kufanya miji duniani ili kuendesha shughuli zake. Ndio maana watu wengi wanaokufa katika mazingira ya kutatanisha “misukule” nao hupelekwa kwenye hiyo miji ya rohoni.

Hata kuzimu ni mji wa rohoni, ambao Yesu alipokufa alishuka kuzimu nakumlaani shetani, kuzimu ni mji wa rohoni.

USHINDI DHIDI YA VIUMBE HEWA.

1. Tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na ng’e na nguvu zote za Yule muovu, wala hakuna kitu kitakacho kudhuru kwa namna yoyote ile.

2. Pia twaweza kuwashinda viumbe wa rohoni kwa kunena kwa lugha mara kwa mara, ambapo unamruhusu Roho mtakatifu akupiganie, hivyo viumbe vya ajabu vitajikuta vinajitenga na wewe.

3. Maombi pia ni silaha Kubwa dhidi ya viumbe vya hewa. Maombi yanalazimisha viumbe hivi kuondoka mahali ambapo walianza kujijenga kwa muda mrefu. Maombi yanauwezo wa kuangamiza ngome.

4. Sisi ni rungu la Bwana ambaolo kwa sisi, Mungu hufyeka farasi na mpanda farasi(viumbe hewa) kumbe hakuna wakufyeka ila sisi tuliookoka.


kunauwezekano wa kuwepo mji kabisa katika ulimwengu war oho kwaajili ya uhalibifu. Kuleta uhalibifu.. katika ulimwengu waroho kuna miji lakini ya rohoni.

Mungu wetu ni Mungu Mtakatifu, wa upendo, hakuna kama yeye.. ni Mungu mkuu mno.. atufunuliaye mambo ya rohohoni maagumu tusiyo yajua.. na wala kuyawazia. MUNGU ANATUPENDA SANA.

Ufufuo na Uzima (The Glory Of Christ (T) Church)
Tanganyika Packers,
Kawe, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment