GOD LOVES YOU/MUNGU ANAKUPENDA

Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

John 3:16 "For God so loved the world that he gave his one and only Son, that whoever believes in him shall not perish but have eternal life.

Friday, September 14, 2012

UTOTO (KIFUNGO CHA UTOTO)

Na Pastor Adriano Makazi:

Unapo kuwa mtoto mdogo unakuwa huwezi kujitegemea kwa jambo lolote lile hadi usaidiwe na mzazi au mkubwa wako aliye kuzidi umri.

Utoto si udhaifu au ugonjwa bali ni hatua ambayo kila mtu ameipitia au anaipitia.

Mfano mzuri tunaona hata YESU mwenyewe alipo vaa mwili alivaa umbo la utoto hii ni kuonyesha kuwa ni lazima hatua hii kila mmoja wetu aipitie.


KUNA AINA TATU ZA UTOTO
1: Utoto wa kimwili. (mwilini)
2: Utoto wa kiroho. (rohoni)
3: Utoto wa akili. (nafsini)

Mtoto wa kimwili anakuwa hajui na hafahamu na hawezi mambo mengi yahusuyo mwili

Mtoto wa kiroho anakuwa hajui na hafahamu na hawezi mambo mengi yahusuyo roho

Mtoto wa akili anakuwa hajui na hafahamu na hawezi mambo mengi yahusuyo kutumia akili(mfano kufikiri, kuwaza, kutafakari, kuamua kwa usahihi n.k)

Kwa kuwa kila kitu kinaanzia kwenye hali ya utoto na kinakuwa taratibu hadi kufikia hali ya utu uzima ndio maana Mungu alituonyesha hili kupitia mwanawe Yesu,jinsi alivyo zaliwa na hadi akakuwa na hatimaye akaanza kazi katika utu uzima.

Watoto huwa wanapatikana kwa uchungu mwingi na maumivu makali,

Angalia jinsi mwanamke azaapo mtoto wake jinsi anavyo zaa kwa uchungu na maumivu makali.

Angalia jinsi Mungu alivyo tuzaa sisi kwa uchungu mwingi kwa kumtoa mwanawe wa pekee Yesu akafa kwa ajili yetu sisi.

Angalia jinsi Yesu alivyo tuzaa sisi kwa njia ya mateso mengi (kupigwa mijeredi,kutemewa mate,kipigiliwa misumari,kuvalishwa taji ya miiba,kufa msalabani,kuchomwa mkuki ubavuni.

Mtoto yeyote azaliwapo anazaliwa akiwa amebeba kusudi la Mungu ndani yake tangu tumboni mwa mamaye.

Mfano=Yesu,Yohana mbatizaji,Yeremiha,Samsoni,Gidioni,Yoshua,Musa n.k


KWA NINI MUNGU ANARUHUSU TUPITIE UTOTO?

  • Kwa sababu ni hatua ambayo kila mtu lazima aipitie ndipo awe mtu mzima baadaye.
  • Kwenye utoto ndio sehemu ya kujifunza mambo mengi na vitu vingi vya aina mbalimbali.
  • Kwenye utoto ndipo tuna jifunza unyenyekevu.
  • Kwenye utoto ndipo tunajifunza utii
Mungu anapo kuweka kwenye utoto anatazamia ujifunze mambo mengi ili uwe mtu ajuae vitu vingi baadaye na uweze kutumika vizuri na yeye.

No comments:

Post a Comment