GOD LOVES YOU/MUNGU ANAKUPENDA

Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

John 3:16 "For God so loved the world that he gave his one and only Son, that whoever believes in him shall not perish but have eternal life.

Thursday, August 30, 2012

Hekima fupi kutoka kwa Mch kiongozi J Gwajima:


kuna mambo manne ili mtu aweze kufanikiwa kwa kingeleza ni 'Break-through'
1. Maarifa
Ukiwa na maarifa aidha ya neno la Mungu au elimu ya kawaida yatakusaidia kupita kwenye eneo ambalo wengine hawawezi kupita, maarifa ni kitu muhimu sana kwenye maisha. elimu ya Neno la Mungu, ufundi au elimu ya darasani. ' mshike sana elimu usimwache aende zake.

2.
Ishi vizuri na watu:
kuishi na watu ni vizuri kwasababu inakutengenezea njia ya kupita, biblia inasema Yesu alikuwa katika hekima na kimo akimpendeza Mungu na wanadamu. kumbe kuwa na mwonekano mzuri mbele ya watu ni jambo zuri kwaajili ya mafanikio.

3. Tabia njema:
mtu anaweza kuwa na maarifa na kipawa lakini akikosa tabia njema hawezi kufanikiwa. mfano mtu ni mwimbaji kaitwa mahali kuimba watu wakapenda lakini tabia ikiwa mbaya hata kile kipawa au elimu yake itadharauliwa.

4. Mpende Mungu kila wakati hata kama hakuna anaye kuuona:
hii ni hatua ya juu sana katika kuumjua Mungu ndio inaitwa kuwa na hofu ya Mungu kwa lugha nyingine ni kumcha Mungu. hii ndio chanzo cha haya mengine biblia inasema 'kumcha Mungu ndio chanzo cha maarifa' na hili jambo ni sahihi.. tenda yanayompendeza Mungu bila kuanfalia nani anakuona!

barikiwa sana............!!!!!

No comments:

Post a Comment