GOD LOVES YOU/MUNGU ANAKUPENDA

Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

John 3:16 "For God so loved the world that he gave his one and only Son, that whoever believes in him shall not perish but have eternal life.

Thursday, August 16, 2012

ROHO YA MWANADAMU na ROHO MTAKATIFU


Mchungaji Josephat Gwajima: Vifungo vya rohoni, Tar. 3.7.2008

Kuna mambo ambayo hekima ya kibinadamu imefungwa kuyafahamu, lakini Mungu anayependa watu wake wawe na maarifa ameyafunua kwetu. Moja wapo ni hili la asili ya roho ya mwanadamu. Tafsiri sahihi ya mtu ni roho yenye nafsi inayokaa ndani ya nyumba inayoitwa mwili. Ukweli ni kwamba mtu sio mwili bali ni roho.

Lengo halikuwa kukupa hiyo tafsiri lakini lengo kuu ni kukufanya ujue kuwa roho yaweza kufungwa. Na kifungo cha roho ni kikubwa kwasababu mafanikio yoyote ya mwilini au nafsini yanaanzia kwenye roho. 3Yohana 1:2, Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. Kumbe roho ikikosa mafanikio hata mwili unakuwa na udhaifu.

Angalau umekaribia kufika ninapohitaji ufike, mambo yote mazuri ya mwilini yanaanzia rohoni. Kwahiyo shetani anachokifanya ni kuifunga roho ya mwanadamu, na matokeo yake tunaona kuwa roho inakosa sauti. Kimsingi roho ikikosa sauti, unaanza kuchukua nafasi, na hapo mtu anaanza kufuata tama za mwilini.  Warumi 8:5-7 “kwa maana wale waufatao mwili huyafikiri mambo ya mwili…” (Wagalatia 5:16-24)   hapo mtu anaanza kutenda matendo ya mwilini, kama kitabu cha wagalatia kilivyoainisha.

Huu ni ugonjwa war oho uliwakamata watu wengi ikiwemo waliookoka, kwasababu 1Wakorintho 10:4 kuna kinywaji cha roho na chakula cha roho, sasa unapoinyima roho yako chakula lazima ifungwe na shetani. Kimsingi roho ni kama mwili inahitaji kulishwa, usipoilisha ujue inaidhoofisha roho yako, na matokeo yake ni kifungo.

Nitakuwa sijafanya haki kama nitaeleza yote bila kutaja jinsi ya kutoka kwenye jambo hili, kama umekoka kuna njia sahihi itakyokufanya utoke kwenye vifungo vya roho, nah ii ni kwa “kunena kwa lugha” unaponena kwa lugha biblia inasema unakuwa unajijenga mwenyewe. (Wakorintho 14:4) kwahiyo unakuwa unaukosesha sauti mwili wako. Tamaa ya dhambi inabadilika na kuwa tamaa ya maombi na kusoma neno.

Hapo roho yako inafanikiwa na kwa mtindo huo hata magonjwa ya mwilini yanaondoka, hutawaza uzinzi, hutawaza disko bali muda wote utauona kuwa wa BWANA. Mtu huyu uwezi kukuta anakuwa na hofu yayajayo, hata ndoto zitabadilika, maneno ya mtu huyu yanabadilika, lakini cha kupokea hapa ni kwamba badiliko la roho linaleta badiliko la mwili, ambalo ndio badiliko la maisha…..

Hope you are blessed!
Vifungo vya rohoni, Tar. 3.7.2008

No comments:

Post a Comment