Yesu aliniita njoo, raha ipo kwangu,
kichwa chako ukilaze, kifuani mwangu.
nilikwenda kwake mara, sana nilichoka,
nikapata kwake raha, na furaha tena.
Yesu aliniita njoo, kwangu kuna maji,
maji ya uzima bure, unywe uwe hai.
nilikwenda kwake mara, na maji nikanywa,
naishi kwake na kiu, kamwe sina tena.
Yesu aliniita njoo, duniani giza,
ukinitazama mimi, nitakuang'alizia.
nilikwenda kwake, mara yeye jua langu,
ni kila wakati mwanga, safarini mwangu.
No comments:
Post a Comment