Imani ni kuwa na hakika ya mambo
yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana (Waebrania 11:1). Kuna
tafsiri nyingi za imani lakini tafsiri hii ni sahihi zaidi. Kwasababu imegusa
maeneo yote, kiufupi ni tafsiri ambayo unapoisoma inakupa mwanga halisi wa
imani!
Biblia
inasema si kwa mafumbo bali waziwazi kuwa imani chanzo chake ni kusikia, kama
hukusikia huwezi kuipokea imani, tena haiishii hapo, inaenda mbali na kusema
kusikia huku kunatokana na neno la Kristo (Warumi
10:17). Kumbe IMANI dhidi ya shetani haiji kwa kusikiliza neno la mganga
bali ni kwa kusikiliza neno la Kristo!
Jambo
lingine, imani pasipo matendo, biblia inafananisha na roho bila mwili (Yakobo 2:26). Kimsingi kabla ya roho
kuingia kwenye mwili, mwili ulikuwa kama sanamu kiufupi (functionless), kama
roho ilipoleta uhai kwenye mwili, ndivyo matendo yanavyoleta uhai kwenye imani.
Waweza kuwa na imani lakini kama haiambatani na matendo ile imani imekufa.
Ili
kupambana dhidi ya huyu mzee kibogoyo au shetani kwa jina maarufu, unatakiwa
uchague uwanja wa kupambania. Na ukishindwa kujua uwanja wa kupigania, kimsingi
unakuwa umeshindwa kabla ya kuanza. Kuna viwanja aina mbili, kwanza cha mawazo
na pili cha imani. Ukipambana na shetani kwenye uwanja wa mawazo, lazima akushindi
kwasababu yuko fiti katika eneo hilo kiufupi ni uwanja wake wa nyumbani.
Ila
uwanja wa imani + matendo yaani unamfanya shetani awe ugenini, alafu hana
washabiki kwa maana hata mapepo wanaelewa ni saa ya kushindwa. Kivipi? Mawazo
yako ndani ya nafsi, na nafsi imejaa yale mambo uliyopitia ambayo ni ya hapa
duniani. Na kama unavyojua shetani kaisuka hii dunia anavyopenda yeye kwahiyo
kukubali kuwa uwanja huo maana yake rahiso ni kuwa uwanja wa ugenini. Lakini
uwanja wa imani ni wa nyumbani, kwanza kwakuwa wenyeji wetu uko mbinguni(Wafilipi 3:20), pili imani yatokana na
neno la Kristo, ambalo limemwagiwa sifa kemukemu (Waebrania 4:12)
Tena Mtaifahamu Kweli,
Nayo Hiyo Kweli Itawaweka Huru (Yohana
8:32)
Hii ni imetolewa kwenye masomo
mbalimbali ya baba yanayohusu IMANI…. Barikiwa!!!
No comments:
Post a Comment