Na Mchungaji: Josephat Gwajima.
Shetani ana mbinu nyingi za kumfunga mtu, na ndio maana Biblia
inasema 2Wakorintho 2:11 “Shetani asije
akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.” Kwa
maana hiyo imetupasa kujua mbinu anazotumia shetani, ili kuufunga mwili wa
mwanadamu. Watu wengi wanasumbuliwa na vifungo vya mwilini, ikiwemo magonjwa
mbalimbali hii ni kwasababu ya kutokujua siri hii, kuwa mwili ni udongo. Sasa
tuone njia ambazo shetani hutumia kuufunga mwili, ambao kwa asili ni udongo, tofauti yake na udongo wa kawaida ni kwamba mwili uliwahi kushikwa na Mungu, pili mwili wa binadamu unauhai unao upata kutoka kwenye roho: njia kadhaa anazotumia shetani...
i)
Kupanda na Kung’oa:
Mhubiri 12:7 “Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho
kumrudia Mungu aliyeitoa.” Kama
tulivyoona toka mwanzo kuwa mwili ni udongo, na kwamaana hiyo, unavyoweza
kuutendea udongo wa kawaida ndivyo hata mwili nao waweza kuutendewa vivyo hivyo
katika ulimwengu wa roho. Kwenye udongo wa kawaida watu hupanda na kung’oa,
kwahiyo na kwenye mwili ambao ni udongo kunaweza kupanda vitu mbalimbali.
Biblia inasema
Mungu ni roho (Yohana 4:24), lakini pamoja na hilo kwamba ni roho aliweza
kupanda bustani katika kitabu cha Mwanzo 2:8 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa
mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.” Ingawa
Mungu alikuwa roho lakini aliweza kupanda bustani, na maandiko mengine
kuonyesha BWANA aweza kupanda (Zaburi 104:16; Hesabu 24:6). Kumbe roho zaweza kupanda na ndio maana
katika Mathayo 15:13 “Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa
mbinguni litang'olewa.” Kumbe kuna mapando ambayo hayajapandwa na
Mungu, na yanatakiwa yang’olewe. Hapa tunafundishwa kuwa kuna uwezekano wa
mwili wa binadamu ambao ni udongo, kupandiwa vitu kama udongo wa kawaida.
Ayubu 4:8, Shetani ni mkulima analima maovu, na kupanda madhara. Mwili wa binadamu unaweza kupandiwa mmea au
mti. Na ndio maana mtu anaweza kuwa safi rohoni na nafsini, lakini kumbe kwenye
mwili wake amepandiwa vitu. Kwa namna hii shetani amefunga miili ya watu wengi
sana bila ya wao kujua, ukifunguliwa macho ya rohoni ukaona utagundua kuwa watu
wengi wamefungwa kwa jinsi hii. Na biblia inasema kwa muda nchi idumupo majira
ya kupanda na kuvuna hayatakoma (Mwanzo 8:22), hivyo dunia imekaa
katika kupanda na kuvuna.
Tunaweza
kujifunza zaidi katika hili, kwenye Mambo ya walawi 19:19 “…usipande shamba
lako mbegu za namna mbili pamoja;…” utajiuliza kwanini Mungu
aliyasema haya kwenye torati, kimsingi torati asili yake ni ya rohoni Warumi
7:14 “…torati
asili yake ni ya rohoni;…” sasa basi hayo Mungu aliagiza kuonyesha
kuwa kuna uwezekana kwenye udongo kukapandwa pando la kiMungu au la shetani. Maana ya maneno haya ni kwamba pale ambapo
Mungu amepanda shetani hatakiwi kupanda, Mfano, Ukiokoka Mungu anakupandia
mbegu ya amani, upendo, furaha na afya. Hapo shetani hatakiwi kupanda mbegu
yake, na hapo andiko la kila pando asilolipanda Mungu, litangolewa linapoleta
maana.
Asili mia kubwa
ya magonjwa yanayowapata watu, ni matokeo ya mapando ya rohoni. Mtu anaweza
akawa anaonekana kwa nje amepooza kumbe kwenye mwili wake amepandiwa mti. Na
pepo wamekaa kwenye mwili wake kama mti.
ii)
Pepo anaweza kugeuka na kuwa:
Shetani
na mapepo wachafu wote ni roho, na wanafanya kazi katika ulimwengu waroho. Na
kwa hivyo kuna sifa ambazo wanazo zinazowatofautisha na wanadamu ojawapo ni
uwezo wa kujibadilisha kwenye maumbo mbalimbali. Ukisoma kitabu cha 1wafalme
22:19-23 “…Akatokapepo, akasimama mbele za
Bwana, akasema, Mimi nitamdanganya. Bwana akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka,
na kuwa pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na
kudiriki pia; ondoka ukafanye hivyo...” Tunaona huyu pepo, hakuwa
pepo wa uongo lakini aliweza alijibadili na kuwa pepo wa uongo. Kumbe kimsingi
shetani na mapepo yanaweza kujibadili na kuwa umbo wanalotaka.
Kama tulivyoona kuwa mwili wa binadamu ni
udongo, na kwenye udongo waweza kuchoma vitu kama kisu, kunawanyama wanatambaa,
mimea inaota na hatakuchimba shimo. Hivyo mapepo wao wapo katika ulimwengu wa roho kwahivyo wakiuangalia mwili wanaona ni udongo kabisa, sasa wanapotumwa na
mchawi au mganga wa kienyeji, wanakuja na kujiuza na kuwa kitu kile
walichotumwa kufanya. Mfano, waweza kumkuta mtu analalamika kuwa kuna vitu
vinatembea kwenye mwili, kumbe ni pepo kajigeuza akawa mnyama atambaaye, mtu
anawashwa mwili kumbe mmea wa upupu au mwili unachoma kumbe pepo kajigeuza na
kuwa kisu. Shetani yupo na anatenda kazi
ya kufunga miili kwa namna hiyo.
Pepo anaweza kujibadili na kisu cha kuchoma
moyo, na matokeo yake utamwona mtu huyu anakuwa na uchungu au anakosa amani
kila wakati. Jambo linaweza kuwa dogo tu lakini likamuumiza sana moyo, kumbe
kuna pepo aliyejibadili na kuwa kisu. Kinachofanyika ni kwamba pepo ametumwa na
kunuiziwa awe kisu, hivyo anabadilika na kuwa kisu kwenye moyo ili usione amani
kwenye maisha. Na watu namna hii wasipopata msaada wa haraka hufikia kujiua.
iii)
Kufunikwa
uso:
Kama tulivyoona kuwa pepo aweza kujigeuza na
kuwa. Njia hiyo shetani huitumia kufunika uso. Na ndio maana mtu anawezasema
ana roho ya kukataliwa kumbe pepo amekuja usoni na kujigeuza kuwa sura nyingine
kabisa. Na mpo mtu mwingine anapoongea naye yaani hisia tu zinakuja, kuwa anaongea na kitu kingine, kwa njia hiyo
watu wanaanza kujitenga naye. Kumbe ni pepo aliyejigeuza na kuwa uso bandia.
Tabia ndiyo ambayo Yule pepo kwenye kitabu cha (1wafalme
22:19-23). Alivyofanya. Kumbe unaweza kumuona mtu
anatukana matusi ya ajabu kumbe pepo kajigeuza kuwa kinywa chake usoni. Mapepo
waweza kujigeuza maumbo mbalimbali, kama nyani, samba, paka hata bundi ilimradi
kuharibu hatma ya mtu. Mnamkuta dada aolewi kumbe uso wake umefunikwa kwa sura
ya simba, kila mwanaume anayetaka kumchumbia haoni sura nzuri bali anaona simba.
Na ndio maana kuna baadhi ya wadada watumia muda mwingi kufanya kujipodoa
lakini bado, kumbe wamefunikwa.
"KWA KUSUDI HILI MWANA WA ADAMU ALIDHIHILISHWA, ILI AZIVUNJE KAZI ZOTE ZA IBILISI"
barikiwa.....
No comments:
Post a Comment