UTANGULIZI:
Kila jambo lina nguzo linazozitegemea, na kila utawala una
nguzo unaotegemea.. vilevile utawala washetani umejengwa juu ya nguzo ziitwazo
MAUTI na KUZIMU.. Ayubu 38:18 na nguzo hizi mbili ndizo ambazo zinashikilia
utawala wa shetani na ndio maana maeneo mengi ambayo kuzimu inatajwa basin a
mauti ipo pia.. mfano katika kitabu cha zaburi 116 :3 .. HAPA UTAONA kila
mahali ambapo mauti imetajwa basi kuna mahusiano na kuzimu .
MAANA YA MAUTI NA
KUZIMU:
Mauti ni roho ambayo kazi yake ni kuuondoa uhai
ulio ndani ya mtu. Na KUZIMU ni roho
ambayo kazi yake ni kuwahifazi wale waliokufa.. ufunuo 6: 9, Isaya 28 :15
..
Mauti ni roho yenye
akili na yenye kupanga.. ndio maana wanafunzi wa Yesu , walipomuona Yesu yuko
juu ya maji, biblia inasema wanafunzi wa Yesu wakadhani wameona roho.. kumbe
roho ina personality ina akili kili, inaweza kupanga na kutekeleza na pia
yaweza kumpagaa mtu. Kwahiyo mauti ni roho yenye personslity hapo tunaweza sema
mauti ni mtu.. Tunaweza sema mauti ni mtu ina “personality” ufunuo 20 : 13.. mauti inaweza
kumeza watu..
ufunuo 20 : 14 kila mahali inapotajwa mauti kuzimu inafuata
pale, hii inaonyesha kuwa mauti inaanza alafu kuzimu inafuata.. katika hiki kitabu cha ufunuo 20 : 14 tunaona
kuwa “ mauti na kuzimu vikatupwa kwenye jehanamu” kumbe mauti unaweza uka
ikamata kabisa na kuitupa mahali.. kama mauti na kuzimu vingekuwa ni matukio
basi visingeweza kushikwa na kutupwa kwenye moto. Ndio maana Yesu alipokufa alishinda
mauti na kuzimu. ( yohana 20 :3)
tuangalie hili andiko mwanzo 37:25 katika agano la kale kuzimu lilikuwa
linatumika kama mahali wafu walipokuwa wanakwenda, na palikuwa panaitwa “sheol”
kwa lugha ya kingereza na huko wako wafu wote waliotenda haki na walitenda
maovu walikuwa wanakwenda kule.. lakini palikuwa wamepagawa mahali pa watenda
haki na mahali pa watenda maovu.. na mahali walipokuwa wanaenda watenda palikuwa
panaitwa Kifuani pa Ibrahimu, ( yaani wale walioamua kuungana na imani ya
Ibrahim) na sasa kunaitwa paradiso..
TOFAUTI YA JEHANAMU
NA KUZIMU:
Jehanamu ni shimo la rohoni la moto watakapo angamizwa watu
watendao dhambi, kwasasa jehanamu hakuna mtu ndani maana hukumu bado
haijatolewa lakini watu wanaokufa
kwa sasa wanaenda kuzimu (bottomless
pit) hii ni roho iliyojifunua kama shimo.
Isaya 14:11,15 . tunaona shetani alipoasi akatupwa kwenye hilo shimo
ndio maana ya maneno yaliyo katika kitabu cha ufunuo 12:7-9 kumbe kuzimu ipo
hapa katika nchi, hapaonekani kwa kuwa lipo katika ulimwengu wa roho. Ufunuo
9:15 , KUZIMU ndio kwenye makao makuu ya shetani , wanakofanyia kazi zao..
(operation centre) ufunuo 17:8 .. kwa hiyo ni muhimu kujua kuzimo ipo angani,
baharini na hata kwenye nchi.. ndio maana biblia inataja mara nyingu neon hili
wakuu wa anga’
KAZI ZA MAUTI NA
KUZIMU:
Hapo mgonjwa anapokuwa dhaifu ndipo sasa mauti inakuja na
kufanya kazi yake, ya kumuua . na mauti ikifanikiwa kuutoa uhai basi sasa mauti
inatuma mapepo wa kuja kumchukua Yule mtu kama alikuwa mtenda dhambi.. na ndio
maana utaona kuwa mtu anapotaka kufa waliowengi utawasikia wanasema maneno kama
‘naona giza’ au msinichukue’ basi ujue wakati huo.
Kuzimu inaleta duniani hata mitindo ya kuvaa.. ili kuingiza tamaa za uzinzi na uasherati..
na unapoona tamaa ya dhambi inaongezeka basi jua unakaribia kufa.. kama
ulipangiwa kuishi miaka 80 utajikuta unaishi miaka 40.. kwa maana mshahara wa
dhambi ni mauti.
Tumepewa mamlaka
dhidi ya mauti na kuzimu, tukiomba kwa Jina la Yesu tunaweza kusambaratisha
mauti na kuzimu. LUKA 10:19
UFUFUO NA UZIMA(THE GLORY OF CHRIST (T) CHURCH)
TANGANYIKA PACKERS,
KAWE, DAR ES SALAAM.
Good job Pastor!
ReplyDeletethanks, May God bless you for visiting... if you have something encouraging dont hesitate to send it through my email.. :dmgongolwa@gmail.com and i will post..
ReplyDelete