GOD LOVES YOU/MUNGU ANAKUPENDA

Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

John 3:16 "For God so loved the world that he gave his one and only Son, that whoever believes in him shall not perish but have eternal life.

Tuesday, August 14, 2012

IMANI INAYOKUWEZESHA KUISHI



Katika biblia kuna maandiko maarufu yaani yanayojulikana sana, na mojawapo linatafsiri imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo.kama una taraja lolote, Imani ndiyo inayoweza kukupa hilo taraja lako.



Imani inakupa sababu ya kumiliki kitu kabla ya kukiona kwa macho ya nyama. Kwanini? Kwasababu Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, Inayataja kuwa halisi, yale mambo ambayo kwenye ulimwengu wa mwili hayaonekani. Lakini imani unayataja kana kwamba yameshafanyika.



Imani pia inatafsiriwa kwenye Biblia kama bayana ya mambo yatarajiwayo;  yaani ni bayana ya ukweli usioonekana. Siwezi kuyaona mambo hayo kwa macho ya kawaida lakini ni bayana kwangu.Ni bayana kiasi kwamba uwezi kuyachukua kutoka kwangu. Hii ndio imani.



Imani ni bayana ya mambo yasioonekana. Hii inamaanisha kuwa imani ni ushahidi wa kiwepo kitu ambacho huwezi kukihisi kupitia milango ya fahamu, Imani ni hati-miliki. Mfano: Umenunua kiwanja, uwezi kukibeba hiko kiwanja ukatembea nacho kila mahali, kuwaonyesha watu. Badala yake unapewa Haki-miliki, kwa mujibu wa kamusi hakimiliki ni taarifa au mkataba wa kisheria unaoonyesha ushahidi wa umiliki. Kama mtu atahitaji ushahidi wa umiliki wako, hapo utatoa hati-miliki badala ya kutembea na kiwanja chenyewe kuthibitisha umiliki. Hiyo ndio maana ya bayana ya mambo yatarajiwayo.



Ni kweli kile kiwanja kipo lakini kwa kuwa huwezi kubeba na kutembea nacho, sasa ukitaka watu wajue kama unakiwanja, unachokifanya ni kuwaonyesha hati miliki. Ambayo wakiiona hiyo wote watajua fika kwamba kiwanja kipo.



Imani haiusiani na milango ya fahamu, Kwasababu ni bayana ya ,mambo yasioonekana kupitia fahamu zetu.pia imani inapita fakra na uwezo wa kufiri wa kibinadamu. Imani ni nguvu ya rohoni; ambayo inasukumwa na roho. Na ndio maana napenda kuitafsiri imani kama MWITIKIO WA ROHO UNAOKUTOKANA NA NENO LA MUNGU!!!

No comments:

Post a Comment