GOD LOVES YOU/MUNGU ANAKUPENDA

Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

John 3:16 "For God so loved the world that he gave his one and only Son, that whoever believes in him shall not perish but have eternal life.

Monday, August 13, 2012

Tofauti iliyopo kati ya Dini na Wokovu!!!

Tofauti kati ya Dini na Wokovu ni moja kuu..:

Dini ni mpango wa wanadamu kumtafuta Mungu, kipindi ambacho Mungu aliuficha us wake kwasababu ya uovu, wanadamu wakaanzisha dini mbalimbali kwaajili ya kumtafuta yeye!!!

Lakini Wokovu ni mpango wa Mungu kuwatafuta wanadamu, kipindi wanadamu wamekata tamaa ya ukombozi Mungu akamtuma mwanawe pekee Yesu Kristo, Afe kwaajili ya Dhambi za wanadamu. ili wahesabiwe haki kwa Neema yake.

Mimi nina dini, lakini sio itakayonipeleka mbinguni, inanisaidia kunilea katika maisha ya kiMungu tu. lakini kumpokea Yesu moyoni binafsi ndio njia pekee ya kumwona Mungu. Warumi 10:10 kwa kuwa ukimkiri Yesu, kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA na kuamini moyoni mwako Utaokoka.... Mwamini Yesu leo uokoke...

No comments:

Post a Comment