GOD LOVES YOU/MUNGU ANAKUPENDA

Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

John 3:16 "For God so loved the world that he gave his one and only Son, that whoever believes in him shall not perish but have eternal life.

Friday, August 10, 2012

UJUMBE: Ndoto ya Daniel na Siku zetu.

Na Mch. Kiongozi : Josephat Gwajima 11.6.2012

Utangulizi:  
Daniel 2: 24-… Hii ni ndoto aliyoota Mfalme Nebkadneza, na hakujua tafsiri yake, akaamua kuita wenye hekima na watafsiri wa ndoto, lakini hawakuweza. Ndipo Daniel akaitwa ili atafsiri na mwanzo wa tafsiri ya Daniel alianza kuelezea vitu vine vilivyokuwa kwenye ile ndoto kama ifuatavyo :-

MAANA YA SANAMU ALIYOIONA MFALME NEBKADNEZA KWENYE NDOTO:-
·         >Kichwa cha dhahabu safi ni Mfalme Nebkadneza (babeli)
Daniel 2:38
·         >Mikono yake na kifua chake ni cha fedha (mikono miwili na kifua ni cha fedha)
Daniel 2:39
·         >Matumbo na viuno vya shaba
Daniel 2:39
·         >Miguu na vidole yake ni ya chuma
Daniel 2:40-44 “ufalme wan ne utakuwa na nguvu mfano wa chuma..  
·         >Jiwe limechongwa mlimani bila kazi ya mikono
Daniel 2: 44-45“katika siku za wafalme hao….”

MUNGU AKAMLETEA DANIEL NDOTO ILEIE KWA NAMNA NYINGINE.
Daniel 7: 1… Ndoto ambayo Daniel aliiota, maana ya pepo kuvuma ni vita au vurugu duniani, mfano vita ya kwanza ya dunia ilileta makoloni Africa, vita ya pili ilileta umoja wa mataifa..  hata vurugu za uchumi zinazoendelea zinaanda jambo kutokea duniani.
Wanyama aliowaona Daniel:-
·         Daniel 7:4 “Mnyama wa kwanza alikuwa Simba, naye alikuwa na mabawa na tai na mabawa yake yalifutuka manyoya…..
·         Kama Dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwa kinywani mwake katika meno yake….
·         Mnyama wa tatu ni chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kamandege, mnyama huyo alikuwa na vichwa vine, akapewa mamlaka
·         Mnyama wa nne Daniel 7:7-11 : utajiuliza swali kwanini Daniel alipokuwa akiwaelezea hawa wengine, hakuwaelezea sana lakini kwa mnyama wanne utagundua kuwa Daniel alimwelezea kwa undani sana. Na alipohitaji tafsiri aliulizia zaidi huyu mnyama wanne. Utagundua kuwa huyu mnyama wan ne anasiri ambayo kama wakristo tunatakiwa kujua.

TAFSIRI YA NDOTO YA DANIEL.
Tafsiri kwenye Daniel 7:16-… wafalme wakubwa watakaotokea duniani.. Daniel alikuwa makini kujua tafsiri ya Yule mnyama wanne.. aliyekuwa akitisha sana na alikuwa kimwonekano mbali sana na wale wengine. Mstari wa 21 > “ilifanya vita na watakatifu na ikawashinda”.
            Mstari wa 24 “Huyo mnyama atakuwa mfalme wa duniani.. na kwa habari za pembe kumi katika ufalme kumi, wataondoka wafalme kumi na mmoja ataondoka kati ya wale wafalme kumi alafu atawashusha wafalme wengine watatu..

MAELEZO YA TAFSIRI YA NDOTO YA MFALME NEBKADNEZA NA NDOTO YA DANIEL:-
Tuanze na uhusiano wa hizi ndoto mbili:
i.                    Kichwa kilikuwa ni mfalme nebkadneza,
ii.                  Kifua na mikono ni mnyama mwenye mbavu tatu, sawa na kifua na mikono miwili aliyoiona mfalme Nebkadneza. Huu ni utawala wa Umedi na Uajemi ambao ulitawala baada ya ufalme wa babeli uliokuwa chini ya Nebkadneza.
iii.                Matumbo na viuno alivyoona Mfalme Nebkadneza, ni utawala wa kigiriki uliotawala baada ya ya ufalme wa umedi na uajemi.
iv.                 Miguu ni utawala wa kirumi , ambao uliua na kuangamiza wakristo kipindi kile.  Kwasababu kipindi utawala wa kirumi unatawala ndipo kipindi ambapo ukristo ulikuwa unaanza na ndio maana kwa historia ya kawaida tu watakatifu wengi waliuawa kipindi hiki na waliangamizwa na utawala wa kirumi. Na kwa kipindi hiki karibu wote kati watakatifu waliuawa.
Baada ya utawala wa kirumi kuwaua wakristo na watakatifu wa kanisa la kwanza, baada ya Mtawala wa kipindi kile kufa, akaibuka mfalme mwingine aliyeitwa Agustino na ambaye alisema kuwa ameamua kuwa mkristo. Na baada ya kutawala ndipo mfalme agustino akaamua kuunganisha upagani wa kirumi kuunganisha na ukristo ili aweze kutawala na yeye akawa kiongozi wa kwanza kama papa wa kanisa katoliki. Na akaamua kuingiza mambo ya kiserikari kwenye ukristo.na ikaingia mambo ya salamu mari, na rozali hapo ambazo hapo awali hazikuwepo kwenye ukristo.
Na ndio maana tangu karne ya nne ukatoliki ukatawala katika ulaya na duniani, ukiingia kama dini na serikari, na waliendelea mpaka karne ya kumi na sita. Ambapo mtu mmoja aliyekuwa anaitwa Martin Luther, akaamua kutoka kwenye ukatoliki akipinga msamaha kutolewa kwa hela na akaamua kuanzisha kanisa linaloitwa Lutheran. Na pia kipindi kile Mfalme wa uingereza alibadili na kuanzisha kanisa lililoitwa Supreme Church Of England. ambalo linaitwa Anglikana, likitokana na nchi ya uingereza. Na padre mmoja mtu mmoja nayeitwa Peter Cameron akaanzisha Inland Church, akatoka mtu anaitwa Simon Menon na dini hiyo ikaitwa Menonite, na hapo wakaibuka mtu aliyeitwa Morovin na kanisa lake likaitwa Morovian.
      Ni Muhimu kujua Dini ni mpango wa wanadamu kumtafuta Mungu..

MATAIFA KUMI NA YALIYO INUKA.
            Daniel aliona mataifa kumi na pembe tatu zikaanguka, tunapoona umoja wa ulaya ulianzishwa na nchi kumi ambazo ndizo mama zilizotoka kwenye utawala wa kirumi, na baada ya kuanguka na kugawanyika, lakini tunaona zile pembe tatu zilianguka na kuinua pembe moja.. yenye nguvu, na kama unavyoona duniani kwa sasa nchi kubwa zinalegalega kiuchumi. Huu ni upepo unaolenga kuandaa kumleta mpinga kristo.

PEMBE ILIYOINUKA.
            Huyu ni mpinga kristo ambaye atakuja kurekebisha uchimi wa dunia na kuzima upepo wa kisiasa duniani, na mpinga kristo atatokea ulaya na kwasasa ulaya inamwandaa kutawala duniani. Na huyu atakuwa shetani anayevaa mwili wa mtu duniani.. na kutumia huo kuitawala dunia na kuwa kama Mungu duniani. Hizi vurugu za uchumi na tetesi za vita zinajiindaa kumkaribisha mpinga kristo duniani.

JIWE LISOLOFANYWA KWA KAZI YA WANADAMU.
            Ukifatilia kwa makini utagundua kuna uamsho unaoanza duniani na unaanzia Tanzania, jiulize nchi ya Tanzania kwanini ina mlima mrefu kuliko yote Afrika na  Ziwa lenye kina kirefu kuliko yote lipo hapa. Utapata kujua pia Tanzania imetoa wapiganaji waliomwaga damu kwaajili ya kuwakomboa raia wengine wa duniani. Na viongozi wengi wametokea Tanzania mfano, Mseveni, Kabila, Mbeki n.k.
            Kabla ya mpinga kristo kukaa kwenye kiti chake, lazima uamsho uanze, Mungu ameinua Ufufuo na Uzima kuitikisa dunia. Ufufuo na uzima italazimisha tawala za dunia kuwa na tawala za mwana kondoo.

UFUFUO NA UZIMA (THE GLORY OF CHRIST (T) CHURCH)
TANGANYIKA PACKERS,
KAWE, DAR ES SALAAM.

No comments:

Post a Comment