MSTARI WA KUKUMBUKA: Mathayo
8:28 “Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo
walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia
njia ile.”
Utangulizi:
Mathayo 8:23-32.. “..Naye alipofika
ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye,
wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile…” habari hii ya kwenye kitabu cha Mathayo, imeandikwa pia na
Marko, waandishi hawa ni tofauti lakini habari ni ileile. Kwahiyo kila mmoja
ameandika kulingana na alivyoshuhudia tukio lile. Marko 5:1-10’ “Akamsihi
sana asiwapeleke nje ya nchi ile.” Hii ni kwa mujibu wa Marko, naye
ameandika hadi jina la wale mashetani waliokuwa ndani kama Legioni. Tuone Luka
8: 26-36 , Luka anaanza kueleza kuwa Yule
mtu ni mwenyeji wa mji ule, Luka 8:31 “Wakamsihi
asiwaamuru watoke kwenda shimoni.”
LEGIONI (JESHI)
Legioni maana yake ni kundi la wanajeshi zaidi ya elfu kumi, wenye
silaha na wanatenda kazi kwa ushirikiano. Nao wanashughuli mbalimbali za
kijeshi. Marko 5:9 “Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni
Legioni, a kwa kuwa tu wengi.” Kwahiyo ndani ya Yule mtu kulikuwa na jeshi la
mapepo, ndani yake.
MJI WA DEKAPOLIS:
Huu ni mji ulikuwa na miji ndani yake kumi, nah ii ilikuwa Tafsiri
yake. Nna hiyo miji kumi kwa ujumla ilikuwa inaitwa Dekapolis. Hii miji ilikuwa
na utajili sana, unaweza kujua kama lilikuwa tajiri katika karne ya kwanza, kwa
uwepo wa nguruwe ambao hawakuwepo kwa wayahudi. Na kwa kuwa ulikuwa mji wa
biashara, watu wengi kutoka sehemu tofauti mbalimbali waliishi pale.
Kulikuwa na njia kuu inayokwenda kwenye hiyo miji, na njia hiyo
ilikuwa inapita makaburini. Kama tulivyosoma kwenye kitabu cha MATHAYO, pale
njia kulikuwa na watu wawili wana mapepo wakali mno, hata mtu asiweze kupita
pale. Yaani lile pepo lilikuwa na uwezo wa kuruhusu mtu kupita au kutokupita.
TAFSIRI YA JAMBO HILI:
Yaani katika huo mji ndio kuna biashara na mafanikio, lakini pepo
yupo ndani ya mtu na anaruhusu nani apite na nani asipite. Kama tulivyoona haya
mapepo yalikuwa ni jeshi, lenye mbinu za kuzuia watu (legioni) na ndio maana
walipomuona Yesu anataka kupita wakajitokeza ili wamzuie asipite.
Na ndio maana unaweza ukajaribu kuomba kazi mahali, ukakuta Yule anayetakiwa
kukupa kazi, hatoi kibali sio kwasababu huna vigezo bali ni pepo yuko ndani
yake. Anayechagua nani apite na nani asipite. Hili jambo ni bayana kuna
mashetani kazi yao ni kukuzuia usiende unapotakiwa kwenda. Na ndio maana
unaweza kuona kuwa wale wachungaji wa nguruwe waliruhusiwa kuchunga bila kuwadhuru,
lakini Yesu alipoamua kupIta wakaja kumzuia.
VITA YA BAHARINI:
Wakati yesu alipowambia wanafunzi wake waende kwenye mji wa
Dekapolisi, jambo la ajabu likatokea baharini. Mashua waliokuwa wamepanda
ilitaka kuzama (Marko 4:36-41). Utajiuliza hili jambo ni bahati mbaya, hili
halikuwa bahati mbaya ni wale mashetani
waliokuwa ndani ya yule yalimuona Yesu akiwa anakuja, hivyo wakamletea dhoruba
ili wamuangamizi. Jambo hili linatufundisha kuwa shetani anaye kuzuia yuko
tayari kumshambulia mtu anayetaka kukupa msaada.
ALIYETUMWA KUKUTESA:
Utawala wa shetani upo katika ngazi tofauti, yaani kuna shetani wa
ngazi tofauti, kuna waliokatika ngazi ya majoka, ambao wao walishuka pamoja na
shetani kutoka mbinguni, na wengini ni majini ambao ni mapepo wanaotokana na
desturi za kiarabu. Na ndio maana yale mapepo yalimwomba Yesu asiwatoe kutoka
katika ule mji. Yaani wametumwa kabisa ili kukutesa.
Haya mateso yalikaa ndani ya wale watu ili kuwatesa katika maeneo
tofauti:
>Anakaa uchi:
Na ndio maana waweza kuona mtu anavaa nguo nusu uchi, kumbe ni
pepo amewekwa ndani yake, huyu mtu alikuwa uchi makaburini. Mapepo yaweza
kumfanya mtu akose maadili. Mtu anabadilika tabia kumbe ni msukumo wa kipepo.
>Anajikatakata kwa mawe
>Hakai nyumbani, anakaa mlimani makaburini.
Na ndio maana unaweza kumwona mtu, hatulii. Kumbe pepo limewekwa
ili maisha yasitulie yaani ukipata kazi hudumu kwenye hiyo kazi. Kumbe asilimia
kubwa ya matatizo ya ndoa, biashara, masomo na hata magonjwa, yanasababishwa na
mapepo yaliyotumwa kukutesa.
Tumia mamlaka ya jina la YESU, kuharibu kazi za aliyetumwa
kukutesa, Tumepewa mamlaka dhidi ya mashetani wanakuja kututesa, tumia mamlaka.
Kwa jinala Yesu.
UFUFUO NA UZIMA (THE GLORY OF CHRIST (T) CHURCH)
TANGANYIKA PACKERS,
KAWE, DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment